Lyrics

"Klabu ya soka ya nchini Tanzania Simba Sports Club hatimaye imefudhu hatua ya makundi ligi ya mabingwa Afrika baada ya kushinda mechi yao dhidi ya Primeiro De Agosto ya nchini Angola kwa jumla ya mabao manne kwa moja. Ushindi huu wa Simba ni baada ya kucheza mechi mbili kwa maana ya mechi ya ugenini pamoja na mechi ya nyumbani. Mechi ya ugenini ni baada ya Simba kwenda nchini Angola na kushinda mabao matatu kwa moja na mechi ya marudiamo iliyochezwa katika uwanja wa Mkapa na Simba kuondoka na ushindi wa bao moja kwa sifuri.

Katika mechi ya marudiano Wekundu wa Msimbazi walifanikiwa kupata bao lao katika kipindi cha kwanza katika ile dakika ya thelathini na tatu ya mchezo bao lililodumu mpaka kutimu kwa kipindi cha pili cha mchezo baada ya Moses Phiri mshambuliaji kutokea Zambia kuliweka kambani.

Ukiwa ni mchezo ambao Simba walipata unafuu baada ya kuingia kifua mbele na mabao matatu umiliki wa mpira wa Simba ulikuwa wa asilimia sitini na nne huku Primerio De Agosto wakimiliki mpira kwa asilimia thelathini na saba. Kona jumla zilikuwa nane na Simba walipata jumla ya kona sita huku De Agosto wakiwa na kona mbili pekee.
View more

Mdundo.com is one of Africa's leading music services! The company aims to provide Africa with easy and legal access to online entertainment and reach millions of people across Africa every month. Mdundo enables artists to keep track of fans, downloads and royalties paid in July and January every year.

By downloading MP3 music from Mdundo.com YOU become part of supporting African artists! You can get the latest music, top mixes and your favorite playlists from top artists across Africa. Mdundo also gives you easy access to the hottest podcast, sports and religious content.

Mdundo is also working with top partners across Africa including Vodacom, MTN, Airtel, Safaricom, Universal Music, Warner Music, Opera and many more to make music accessible for all. Mdundo.com A/S is a publicly listed company and Nasdaq First North Growth Market in Copenhagen, Denmark.

I am a musician! - Log in or Sign up