TFF Yatupilia Mbali Shauri la Feisal -Mdundo Alt

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Stella Julius

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania (TFF) limetupilia mbali mapitio ya shauri lililoombwa na Mchezaji Feisal Salum dhidi ya klabu ya soka ya Young Africans sports club katika kikao kilichofanyika siku ya tarehe 2 Machi 2023.

Katika kikao hicho mawakili wa pande zote mbili waliwasilisha hoja zao huku Fatma Karume akiwa miongoni mwa mawakili waliowasilisha hoja zao kwa upande wa Feisal.

Mapitio ya shauri Hilo yalifanyika mara baada ya sakata lililozua utata juu ya mchezaji Feisal ambaye alihitaji kuvunja mkataba na klabu hiyo ya Wananchi. Lakini pia klabu hiyo iligoma baada ya kusemekana kuwepo kwa baadhi ya vipengele vya kimkataba ambavyo vinamlazimu kiungo huyo kusalia Yanga mpaka mwisho wa mkataba wake mwaka 2024.

Taarifa iliyotolewa na TFF ilisema ya kuwa …..Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili kamati imeona kwamba shauri hilo la mapitio (Review) halina msingi wa kisheria kushawishi kamati kubadili maamuzi yake yaliyotolewa awali na hivyo imetupilia mbali shauri hilo …..

Tangu mwezi Desemba Feisal Salum Abdallah hajajihusisha katika michezo yoyote ya klabu hiyo na soka ijapokuwa ameoneoana akifanya mazoezi binafsi sehemu mbalimbali ikiwemo Dubai.

Pia TFF katika taarifa yake hiyo imeeleza ya kuwa ifikapo Jumatatu ya Machi 6 mwaka 2023 itatoa ufafanuzi wa kiundani juu ya shauri Hilo.

Leave your comment