Ubashiri Mechi ya Manchester City Vs Newcastle United -Mdundo Alt

[Picha: Skysports]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Manchester City wakiwa katika safari Yao ya kutetea ubingwa wa ligi ya Uingereza wakiwa nafasi ya pili wanakutana na Newcastle United ambao wako katika nafasi ya tano katika ligi hiyo katika nyasi za uwanja wa Etihad Jumamosi hii

City kwa sasa tamaa Yao iko katika kupata alama tatu katika kila mchezo wa ligi kutokana na hali ya The Gunners kuwa vinara wa ligi na kwa sasa wakiwa na tofauti ya alama Tano pekee.

Pia kwa Wana Hawa wa kasri la mfalme wako pia katika mbio za kombe la ligi ila pia haitakuwa tabu sana kama wakifanikiwa kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa kama watafudhu katika zile Timu nne kwa msimu ujao.

Mbali na hilo Bado Newcastle wako katika majeraha mazito kutokana na kichapo walichopatiwa na mashetani wekundu kwa kunyang'anywa tonge mdomoni katika fainali za Carabao licha ya kuwa na mchezo mzuri katika fainali hizo.

Katika mchezo uliopita Newcastle wakiwa katika viunga vya nyumbani vya Saint James' Park walishuhudiwa wakipata sare ya bao 3-3 hivyo Mwalimu wa kikosi hicho Eddie Howe katika mchezo huu dhidi ya City pia anauwezo wa kupata matokeo chanya japo kwa asilimia chache.

Ubashiri wa Newcastle kupoteza au kutoa sare ni 1.14

Leave your comment