Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
Achraf Hakimi Kutalakiana na Mkewe Hiba- Mdundo Alt
14 April 2023

[Picha: Instagram]
Mwandishi: Stella Julius
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram
Beki anayekipiga League 1 katika timu ya Paris Saint Germain, Achraf Hakimi amefikishana mahakamani na mkewe Hiba Abouk katika shauri la kudai talaka lililoombwa na mkewe huyo.
Katika shauri hilo, Hiba aliiomba mahakama kupatiwa nusu ya umiliki wa mali kutoka kwa mumewe baada ya kukamilika kwa hatua zote za kisheria lakini cha ajabu mahakama imegundua ya kuwa Raia hiyo kutokea nchini Morocco hana mali zozote anazozimiliki kwa sasa.
Uchunguzi huo wa mahakama ulibaini ya kuwa kwa muda mrefu sasa Achraf Hakimi amekuwa akimpatia mama yake mzazi Sadia Mouh umiliki wa mali zake kwani hata mshahara wake kutokea PSG ni asilimia 20 pekee ndizo zinaingia katika mfuko wake huku asilimia 80 zote zikienda kwenye akaunti ya mama yake mzazi.
Mbali na hilo pia mali zingine kama vile vito vya thamani, magari pamoja na nyumba vyote viko chini ya mama yake Achraf na endapo atahitaji kitu chochote huwa inamlazimu kuomba kutoka kwa mama yake.
Achraf pamoja na Hiba walikutana miaka mitano iliyopita na kuamua kufunga ndoa huku wakibarikiwa watoto wawili. Kwa sasa Achraf ana miaka 24 huku mkewe Hiba akiwa na Miaka 36 huku ndoa yao hiyo ikiwa kama jua la jioni linaloelekea kuzama.
Weekly Top 10 songs

In My Bed2:50
KAPEKE LONDON2:23
BIkola2:58
Buwooma2:44
Baddie remix feat Shannnon, aaronix, Tojo3:14
Paver2:55
Nitampeleka kwa Mama (ft. Xouh)3:44
Ex Nkubilako ft DonMusa2:55
CHAMPION GAL3:00
Kamwambie3:47
Top stories
- UPCOMING EP FROM EMKAY64
14 May
- Daniel Sifuna
14 May
- Generation
16 May
- NEW SONG ALERT
16 May


Leave your comment