Sadio Mane amshambulia Lorey Sane -Mdundo Alt

[Picha:sky sports ]

Mwandishi: Stella Julius

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Mchezaji wa Bayern Munich Sadio Mane ameripotiwa kumshambulia mchezaji mwenza wa timu hiyo Leroy Sane mara baada ya mchezo wao dhidi ya Manchester City kukamilika kwa ushindi wa bao 3-0 ushindi walioupata City katika uwanja wa Etihad.

Kipigo hicho kilipelekea mchezaji huyo kutokea na damu na pia wechezaji wengine wa timu ya Bayern Munich ndio waliofanikiwa kuwatenganisha wachezaji hao wakati walipokuwa katika chumba cha kubadilishia nguo.

Pengine hii inaweza kuwa taarifa ya kushtukiza iliyotolewa na Sky Germany kutokana na tabia ya Sadio Mane ambaye ni mchezaji asiyekuwa na taarifa za magomvi pamoja na kipindi hiki kikiwa ni kipindi cha Mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo naye Mane ni Muislam.

Baada ya kurejea Ujerumani inasemekana wawili hao walitenganishwa kwa Sane kuondoka na basi la timu huku Mane akichukuliwa na usafiri binafsi.

Katika mchezo huo Manchester City walipata mabao yao matatu kutoka kwa Erling Haaland, Bernardo Silva pamoja na Rodri ukiwa ni mzunguko wa kwanza wa robo fainali ligi ya mabingwa Ulaya, huku mechi ingine ya ligi ya Mabingwa iliyochezwa siku hiyo Inter Milan walifanikiwa kushinda bao 2 dhidi ya Benfica

Leave your comment