International Women's Day 2023:Wadau Yanga Wawakumbuka wanawake -Mdundo Alt

[Picha: Twitter]

Mwandishi: Stella Julius

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Katika kuelekea siku ya wanawake duniani ambayo hufanyika kila tarehe 8 mwezi Machi, wadau mbalimbali wa soka wakiwa pia ni mashabiki wa klabu ya soka ya Young Africans sports club wamejitolea kuwanunulia tiketi wanawake haswa mashabiki wa Yanga.

Ununuzi wa tiketi hizo umefanywa mahususi kabisa katika mchezo wa makundi wa timu ya Yanga dhidi ya AS Real Bamako utakaochezwa katika uwanja wa Mkapa siku ya Jumatano.

Wadau hao wamajitolea kufanya hamasa hiyo kwa wanawake kama Moja ya motisha na kutambua mchango wao mkubwa katika mpira wa miguu nchini Tanzania pamoja na kutambulisha umuhimu wao katika michezo huo.

Katika ununuzi wa tiketi hizo ni zaidi ya tiketi Elfu moja mia nane zimenunuliwa na zitafikishwa moja kwa moja kwa wanawake wote watakaofunga safari na kuelekea uwanja wa Mkapa kushuhudia mtanange huo.

Katika safari ya Yanga nchini Mali matokeo yalikuwa sare ya bao Moja kwa Moja baada ya AS Real Bamako kusawazisha katika dakika za lala salama.

Licha ya hayo yote lakini pia dau la Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan liko pale pale kwa timu za Simba na Yanga kuzawadiwa kiasi cha Shilingi milioni tano za kitanzania kwa kila goli katika michuano ya kimataifa.

Leave your comment