Yanga Yamtaka Feisal Kambini- Mdundo Alt

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Stella Julius

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Baada ya siku chache kupita tangu shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania (TFF) kubatishilisha shauri la mapitio lililoombwa na mchezaji Feisal Salum dhidi ya klabu ya Young Africans sports club, klabu hiyo imemtaka Feisal kuwasili kambini kwa ajili ya kuendelea na mazoezi akiwa na kikosi hicho cha Yanga.

Yanga imeitoa taarifa hiyo siku tatu baada ya TFF kuwapatia mamlaka dhidi ya mchezaji huyo na kumtambua Feisal kama mchezaji halali wa klabu hiyo ya soka.

Katika taarifa waliyoitoa Yanga pia walitoa maelezo ya kuwa endapo kuna timu yoyote inamuhitaji Feisal basi waingie katika mazungumzo na Yanga na kuongeza ya kuwa endapo upande wa Feisal wangehitaji maboresho ya mkataba pia kuna nafasi ya mazungumzo jambo hilo.

Kabla ya taarifa hiyo siku hiyo hiyo ya Jumatatu tayari kiungo huyo alishawasili katika ofisi za TFF kwa ajili ya kupelekea maombi ya kuvunja mkataba uliopo kati yake na timu ya soka Yanga.

Wakati alipokuwa akiwasili TFF mchezaji huyo alipeleka maombi hayo akiwa na wakili wake Jasmin Razack ambaye pia alimsaidia mchezaji Simon Msuva na kufanikiwa kushinda kesi yake dhidi ya klabu ya soka ya Raja Casablanca .

Leave your comment