Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
Waarabu Kuwakutanisha Messi, Ronaldo
5 April 2023

[Picha: Instagram]
Mwandishi: Stella Julius
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram
Klabu ya soka kutokea Saudi Arabia Al Hilal imetuma ombi kwa mshambuliaji Lionel Messi la kutoa ofa ambayo itakidhi mahitaji yake.Kulingana na taarifa kutoka kwa mwanahabari wa masuala ya soka Fabrizio Romano ofa hiyo inaripotiwa kuwa zaidi ya dola za kimarekani milioni 430 kwa mwaka.
Mbali na timu hiyo pia siku chache zilizopita Barcelona nao waliweka wazi kumhitaji mchezaji huyo endapo kama yeye atatamani kurejea klabuni hapo. Kupitia kwa kocha wake Xavi Hernandez Barca walitangaza nia ya kumhitaji mshindi huyo wa tuzo Saba za ballon D'or endapo kama yeye atatamani kumalizia safari yake ya soka mahali alipoanzia.
Endapo Messi atakubaliana na dili hilo la kwenda kukipiga Saudi Pro League, utaleta mwendelezo wa safari ingine ya kukutana na Cristiano Ronaldo anayeichezea Al Nassr ya huko huko Saudi na kuirejesha safari waliyoianzisha La Liga Messi akiwa Barcelona na Ronaldo akiwa Real Madrid.
Mkataba wa klabu ya Al Hilal kwa Messi unaweza kuwa zaidi ya £ 177m ambayo Al-Nassr wanamlipa Cristiano Ronaldo kwa sasa.
Messi kwa sasa ni mchezaji wa Paris Saint Germain, lakini mkataba wake unamalizika msimu huu na atakuwa mchezaji huru katika miezi sita ijayo huku PSG nao wakiwa Bado hawajatoa taarifa zozote
Weekly Top 10 songs

In My Bed2:50
KAPEKE LONDON2:23
BIkola2:58
Buwooma2:44
Baddie remix feat Shannnon, aaronix, Tojo3:14
Paver2:55
Nitampeleka kwa Mama (ft. Xouh)3:44
Ex Nkubilako ft DonMusa2:55
CHAMPION GAL3:00
Kamwambie3:47
Top stories
- UPCOMING EP FROM EMKAY64
14 May
- Daniel Sifuna
14 May
- Generation
16 May
- NEW SONG ALERT
16 May


Leave your comment