Ubashiri mechi ya Raja Casablanca Vs Simba Sc - Ligi ya Mabingwa Afrika

[Picha: Telecom Asia]

Mwandishi: Stella Julius

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Klabu ya soka ya Simba Sc siku ya Alhamisi imefunga safari ya kuelekea nchini Morocco kwenda katika mchezo dhidi ya Raja Casablanca wakitokea nchini Qatar walipokuwa wakifanya mazoezi.

Kuelekea mchezo huu Simba Sc pamoja na Raja Casablanca tayari wameshafudhu katika kundi lao na sasa wanaelekea katika hatua ya robo fainali ligi ya Mabingwa Afrika mchezo utakaochezwa siku ya Jumamosi

Waongoza kundi Green eagles wao wameonesha uwezo mkubwa katika kundi lao kwani mpaka sasa hawajapoteza mchezo wowote katika kundi C lililohusisha timu za TP Mazembe, Viper AC sambamba na timu ya Simba SC.

Kwa upande wao wekundu wa msimbazi wao hawakuanza vizuri baada ya kupoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Horoya AC. Baada ya mchezo huo Simba  walifanikiwa kulipa kisasi dhidi ya timu hiyo kutokea Guinea kwa ushindi wa bao 7-0.

Katika hatua inayofuata Simba wanaingia katika kibarua kizito na timu zilizofanikiwa kupitia hatua ya makundi ni kati ya timu bora zaidi barani Afrika na timu hizo ni kama vile Mamelodi Sundowns Fc, Wydad Casablanca, CR Belouizdad, Esperance  JS Kabylie ambazo tayari wamefanikiwa kufika hatua ya robo fainali klabu bingwa Afrika.

Katika mchezo huu wa Simba dhidi ya Casablanca ni mchezo wa kukamilisha ratiba baina ya timu hizi na odds za Raja Casablanca kushinda au kutoa sare ni 1.10

 

Leave your comment