Real Madrid wawaadhibu Chelsea-UCL- Mdundo Alt

[Picha: sky sports ]

Mwandishi: Stella Julius

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Real Madrid wamezidi kukaza mkanda wao dhidi ya Chelsea baada ya kufanikiwa kuwafunga mabao 2-0 katika uwanja wa Santiago Bernabeu wakiwa katika hatua ya robo fainali ligi ya mabingwa Ulaya.

Hii ni mara ya pili mfululizo kwa mabingwa bao watetezi Madrid kukutana na Chelsea katika hatua hiyo ya robo fainali baada ya msimu uliopita pia kukutana katika hatua hiyo na Madrid kushinda kwa ujumla wa mabao 5-4.

Bao la kwanza kwa Madrid lilifungwa na straika wa timu hiyo Karim Benzema katika kipindi cha kwanza cha mchezo huku bao la pili lilifungwa na Marco Asensio ambaye alitokea benchi.

Mchezaji bora wa mechi hiyo alikuwa ni winga Vinicius Jr ambaye pia alitoa pasi za usaidizi wa magoli yote mawili katika mchezo huo.

Katika kipindi cha pili The blues walimaliza mchezo wakiwa pungufu kutokana na Ben Chilwell kupatiwa kadi nyekundu kwa madhambi aliyomfanyia Rodrygo katika ile dakika ya 59 ya mchezo.

Katika mchezo mwingine wa Nusu fainali ligi ya Mabingwa Ulaya, AC Milan walimchapa Napoli bao moja kwa sifuri wakiwa nyumbani katika viwanja vya Giuseppe Meazza bao lililofungwa na Ismael Bennacer

Leave your comment