Taifa Stars kumenyana na Uganda Jumanne hii

[Picha: Wasomi Ajira]

Mwandishi: Stella Julius

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars inaingia vitani dhidi ya The Cranes timu ya Taifa ya Uganda katika kuiwania nafasi ya mbele zaidi katika mashindano ya AFCONS kwa Sasa wakiwa katika hatua ya makundi.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Misri katika mji wa Ismailia, Taifa Stars walifanikiwa kushinda mchezo huo kwa ushindi wa bao Moja kwa sifuri, goli lililofungwa na Simon Msuva na kuwaweka mbele Tanzania.

Siku ya Jumanne mtanange wa marudiano utapigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Taifa Stars wakiwa nyumbani pamoja na mtaji kifuani wa bao moja dhidi ya Uganda.

Mbali na hilo lakini pia Rais Samia kwa mara nyingine Tena ametoa ahadi kwa ya milioni 10 kwa kila goli litakalofungwa na timu hiyo sambamba na kitita cha shilingi milioni 100 endapo vijana hao wanaoiwakilisha Tanzania watafanikiwa kutinga fainali za mashindano hayo ya AFCONs

Kwa Sasa Taifa Stars wako katika nafasi ya pili kundi F huku kundi hilo likiongozwa na Algeria wenye alama 9, huku Niger wakishika nafasi ya tatu wakiwa na 2 na Uganda wakiburuza mkia kwa alama 1.

Leave your comment