Yanga, ASEC Memosa wamaliza kibabe makundi kombe la shirikisho

[Picha: The Citizen]

Mwandishi: Stella Julius

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Klabu ya soka ya Young Africans Sports club imetinga hatua ya robo fainali kombe la shirikisho barani Afrika mara baada ya kukamisha mchezo wao wa makundi kwa kuwafunga TP Mazembe ya nchini  Kongo kwa ushindi wa bao 1-0.

Wakiwa katika uwanja wao wa TP Mazembe huku Lubumbashi wakongo hao walishindwa kabisha kuing’aza nyota yao kwa kukubali kichapo hicho mara baada ya kuambulia kipigo kingine dhidi ya timu hiyo katika mchezo uliopita kwa kipiiggo cha bao 3-1.

Katika mtanange huo umiliki wa mpira kwa timu  zote ulikuwa nusu nusu na Yanga kuwazidi mbinu Mazembe baada ya  Farid Mussa kutikisa nyavu za wenye nyumba hao wa Lubumbashi

Timu ya Wananchi Yanga wamekalisha mchezo wao wa makundi kwa kuibuka kinara wa kundi  lao hilo wakiwa na jumla ya alama 13 wakifuatiwa na AS Monastir ya nchini Tunisia wakiwa na alama 13.

Hali kadhalika katika hatua ya makundi kombe la shirikishi timu ya ASEC Memosa pia imemaliza hatua ya makundi wakiwa na jumla ya alama 13 na pia Marumo Gallants wakiwa na alama 12.

Leave your comment