Ubashiri Mechi Za Ligi Kuu Tanzania Bara Wikiendi Hii - Mdundo Alt

[Picha: Telecom Asia]

Mwandishi: Stella Julius

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Mwisho wa wiki ndiyo huu na michezo mbalimbali itatimua vumbi katika maeneo tofauti tofauti katika ligi kuu Tanzania bara. Baadhi ya michezo itakayochezwa ni pamoja na ifuatayo

Siku ya Jumamosi katika uwanja wa Mangungu mkoani Morogoro Simba watakuwa wageni dhidi ya Mtibwa Sugar. Katika mchezo huo Simba akiwa nafasi ya pili anakwenda kwa lengo la kutafuta alama zingine ili angalau aweze kujiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kumpiku Yanga ubingwa. Odds za Simba kushinda mchezo huu ni 1.38

Namungo wakiwa katika viwanja vya nyumbani wanakipiga dhidi ya Tanzania Prison katika nyasi za Majaliwa Stadium. Prison kwa sasa wako katika hatihati za kushuka daraja hivyo mchezo wowote kwao ulio mbele yao ni muhimu zaidi. Odds za Namungo kushinda au kutoa sare ni 1.62

Baada ya ushindi wa bao 2 kwa sifuri dhidi ya Mtibwa Sugar, Singida Big star wanasafiri hadi katika Jiji la Tanga kucheza na Coastal Union katika uwanja wa Mkwakwani. Ushindi kwa Singida ni moja ya tiketi za kuitafuta nafasi ya kucheza kombe la shirikisho kwa msimu ujao. Odds za timu kupata magoli ni 2.49

Vigongo wa ligi kuu Young Africans sports club wakiwa katika uwanja wa Uhuru wanakutana na Geita Gold katika safari ya kutafuta alama za ubingwa. Kwa michezo mitatu iliyopita Yanga alifanikiwa kupata alama tatu dhidi ya Geita Gold hivyo odds za Yanga kushinda au kutoa sare ni 2.16

Leave your comment