Lyrics

Manchester United katika uwanja wao wa nyumbani usiku wa Jumatatu hatimaye wameweza kung'ara baada ya kuwafunga Liverpool ushindi wa mabao 2-1 katika uwanja wake wa nyumbani wa Old Trafford. Katika mchezo huo United walitangulia kupata goli la kwanza dakika ya 15 kupitia kwa kiungo mshambuliaji Jadon Sancho ambaye alipata pasi ya usaidizi kupitia kwa winga wake Anthony Elanga. Bao la pili lilipatikana katika kipindi cha pili cha mchezo ambapo Marcus Rashford alipata pasi ya usaidizi wa goli kutoka kwa Anthony Marshall na kuweka kimiani bao hilo katika dakika ya 53. Katika msimu wa mwaka 2021/22 Rashford alikuwa na jumla ya mabao 04 pekee na kuwa moja ya misimu mibovu sana katika soka lake na hili ndilo bao lake ya kwanza kwa msimu huu. Baada ya hayo Jürgen Klopp ndipo akafanya mabadiliko ya wachezaji na kumuingiza Fabio Carvalho katika dakika ya 73 ambaye alichangamsha mchezo Zaidi kwa Liverpool na kuwapa bao moja kupitia kwa mshambuliaji wake Mohamed Salah katika dakika ya 81 ya mchezo. Majogoo hao wa London Liverpool walimiliki mchezo huo kwa asilimia 70 huku United chini ya Ten Hag wao wakitawala mpira kwa asilimia 30 pekee. Huku mashambulizi ya moja kwa moja goli pinzani Liverpool walikuwa na mashambulizi 5 dhidi ya United waliokuwa mashuti 4. Ukiwa ni mchezo uliowapa umiliki Liverpool kwa asilimia kubwa jumla ya Kona waliozipata ni 8 na moja ikazaa bao huku United wakipata kona 6. Kwa upande wa maotea timu zote zilipata maoteo mawili. Kabla ya kukutana na Liverpool United walipoteza michezo miwili mfululizo walipocheza na Brighton pamoja na Brentford ndipo Erik Ten Hag akaamua kusitisha mapumziko kwa wachezaji na haya yaweza kuwa ndiyo matunda yake.
View more

Mdundo.com is one of Africa's leading music services! The company aims to provide Africa with easy and legal access to online entertainment and reach millions of people across Africa every month. Mdundo enables artists to keep track of fans, downloads and royalties paid in July and January every year.

By downloading MP3 music from Mdundo.com YOU become part of supporting African artists! You can get the latest music, top mixes and your favorite playlists from top artists across Africa. Mdundo also gives you easy access to the hottest podcast, sports and religious content.

Mdundo is also working with top partners across Africa including Vodacom, MTN, Airtel, Safaricom, Universal Music, Warner Music, Opera and many more to make music accessible for all. Mdundo.com A/S is a publicly listed company and Nasdaq First North Growth Market in Copenhagen, Denmark.

I am a musician! - Log in or Sign up