Lyrics

"Mabingwa wa Serie A kwa msimu uliopita AC Milan wameshindwa kung’ara katika mechi yao dhidi ya Chelsea kwa kubali kuondoka na kipigo cha bao tatu kwa sifuri. Katika mchezo huo Chelsea wakiwa nyumbani walishuhudiwa wakiwasulubu Milan huko Stamford Bridge.

Bao la kwanza lilifungwa baada ya Wesley Fofana kupokea pasi kutoka kwa Ruben Loftus-Cheek kabla ya dakika ya 38 Fofana kutolewa nje kwa majeraha. Kipindi cha pili kikaanza na dakika ya 56 Pierre-Emerick Aubameyang kufunga bao la pili baada ya beki wa kulia wa Chelsea Reece James kumpatia pasi makini kabisa. Bao la ushindi lilifungwa na Reece James baada ya Raheem Sterling kumsogezea mpira na beki huyo kukamilisha ushindi huo kwa Chelsea.

Wakiwa nyumbani Chelsea walimiliki mpira kwa asilimia 51 ambazo ziliwapa uwezo wa kupata mabao hayo matatu huku AC Milan wakimiliki mpira kwa asilimia 46. Maoteo kwa Chelsea yalikuwa matatu huku Milan wakiwa na oteo moja pekee. Jumla ya kona zilikuwa saba, kona nne zikitokea katika kikosi kazi cha Graham Potter na kona tatu zikitokea katika kikosi cha Stefano Pioli . Kadi zilizotolewa ni tano nazo mbili kwa Chelsea na tatu kwa AC Milan.
View more

Mdundo.com is one of Africa's leading music services! The company aims to provide Africa with easy and legal access to online entertainment and reach millions of people across Africa every month. Mdundo enables artists to keep track of fans, downloads and royalties paid in July and January every year.

By downloading MP3 music from Mdundo.com YOU become part of supporting African artists! You can get the latest music, top mixes and your favorite playlists from top artists across Africa. Mdundo also gives you easy access to the hottest podcast, sports and religious content.

Mdundo is also working with top partners across Africa including Vodacom, MTN, Airtel, Safaricom, Universal Music, Warner Music, Opera and many more to make music accessible for all. Mdundo.com A/S is a publicly listed company and Nasdaq First North Growth Market in Copenhagen, Denmark.

I am a musician! - Log in or Sign up