• Stream Marioo - Shisha Feat. Mr Nice

    Shisha Feat. Mr Nice

    Marioo

    1:21

Mtunzi na mwimbaji wa nyimbo za aina ya Bongo Flava, Marioo, ameachia wimbo mpya wa kusisimua mno unaofahamika kama Shisha. Kinachosisimua mashabiki wa wimbo huu ni kuwa Marioo ameweza kumshirikisha Msanii mashuuri aliyevuma enzi za kale anayejulikana kama Mr. Nice.

Wimbo huu umeiga mfano wa mtindo wa wimbo wake Mr. Nice, King’asti kwa kuchanganya na ladha mpya ya Kisasa ya Amapiano na sampuli ya maneno kutoka kwa wimbo wake Mr.Nice. Japokuwa nyimbo zote mbili, wake Mr. Nice ulio wa asili na huu mpya wa Marioo zinaongelelea mada ya mapenzi kuna kinaya Kwani wimbo wa kwanza uliashiria vile wapenzi wawili walipendana enzi hizo na walikuwa tayari kulilinda penzi Hilo ilhali wimbo wake Marioo unaeleza mapenzi ya kisasa ambapo Msanii anaamini hamna kitu kama mapenzi kamili na kuashiria kuwa upendo anaoufahamu ni wa Shisha tu. Mdundo wa wimbo mwenyewe unavutia Kwani una mvuto unaonata na kumfanya mtu kutaka kudansi au kuskiliza Mara kadhaa kwasababu ya mvuto huo.

Kupata habari zaidi kuhusu muziki unaotamba barani Afrika, tembelea tovuti yetu www.mdundo.com