Nyimbo Mpya Tanzania na Kenya Wiki Hii

Picha Kutoka Instagram
Mwandishi:
Charles Maganga

Ndani ya wiki hii, wasanii tofauti tofauti kwenye kiwanda cha muziki Tanzania wameendelea kupba kiwanda cha Bongo Fleva kwa nyimbo kali zenye mahadhi tofauti tofauti kama Hip Hop, Bongo Fleva na aina nyingine za muziki. 

Kutoka kwa wasanii kama Nandy, Nay Mitego na wengineo wengi, hizi hapa ni ngoma mpya Tanzania wiki hii : 

On Fire - Ali Kiba 

Baada ya kuburudisha mashabiki na “Mahaba” mapema mwaka huu, Ali Kiba amerudi tena na “On Fire” ngoma ambayo Kiba anaeleza kwa undani namna ambavyo penzi limemnogea na namna ambavyo ana furaha kwa sasa.

Falling - Nandy 

Kwenye ngoma mpya ya Nandy utapata mashahiri mujarab ya mapenzi lakini pia utarahani mdundo mkali kutoka kwa Kimambo beats ambaye ndiye ametayarisha “Falling” ambayo ni ngoma ya kwanza kutoka kwa Nandy kwa mwaka 2023. 

Yanga Anthem 2 - Marioo

Marioo kwa mara nyingine aliamua kukosha mashabiki wa Yanga na wimbo wake wa “Yanga Anthem 2” ambao ndani yake fundi huyo Bongo Fleva amesifia haswa klabu ya Yanga ambayo ni moja kati ya klabu za soka nchini Tanzania. 

Tushaachana - Chiby & Mabantu 

Kwenye wimbo huu Mabantu kwa maneno mepesi sana wameeleza dhana ya “Friends For Benefit” ambapo humu ndani wakali hawa wanaweka wazi kuwa wameshaachana na wapenzi wao wa zamani lakini bado wanaendeleza kwa siri mahusiano yao. 

Funga Kazi - Manengo Ft Darassa 

Muziki wa Hiphop ulipata zawadi wiki hii kutoka kwa Manengo akiwa na Darassa kupitia “Funga Kazi” wimbo mkali wa rap ambao ndani yake Manengo na Darassa wanazungumzia mambo mbalimbali ya kila siku. 
"

Leave your comment

Top stories