Diamond Platnumz Na Billnass Waandika Historia Mwezi Machi

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Wasanii kutoka nchini Tanzania Diamond Platnumz na rapa Billnass wameandika historia mwezi Machi baada ya kufanya vizuri kwenye mtandao Youtube kwa mwezi huo.

Diamond Platnumz ambaye kwa mwaka wa 2023 ameshaachia ngoma 2 kwa mara nyingine ameweka rekodi mpya Youtube kwa mwezi Machi huku Billnass akiwa ameongoza kwenye orodha ya wasanii wa Hiphop Tanzania waliofanya vizuri kwenye mtandao huo.

Kwa mwezi Machi pekee Diamond Platnumz amekusanya views Milioni 31 kwenye mtandao na hivyo kuwa msanii wa Tanzania aliyetazamwa zaidi kwa mwezi huo. Kwenye orodha hiyo iliyotolewa na Charts Tanzania Harmonize anashika nafasi ya pili akiwa na views Milioni 14, Rayvanny, Zuchu na Ali Kiba pia waling’ara kwenye orodha hiyo.

Kwa uplande wa Hip Hop Billnass alikusanya views Milioni 2.52 hivyo kuwa Msanii wa Hip Hop aliyetazamwa zaidi YouTube kwa mwezi Machi. Darassa, Stamina Shorwebwenzi, Nay Wa Mitego na Kontawa ni Baathist ya wasanii waliotajwa pia kwenye orodha hiyo.

Leave your comment