Nyimbo Mpya: Zuchu 'Utaniua',Rayvanny 'Forever' Na Ngoma Zingine Mpya Tanzania Wiki Hii

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Ni ukweli ulio wazi kuwa kwa sasa kiwanda cha muziki Tanzania kimechangamka sana na kila siku wasanii wana na kila siku wasanii wanatoa ngoma mpya na kali kwa ajili ya mashabiki kuweza kusikiliza na kwa kulijua hilo tumekuwekea orodha ya ngoma 5 mpya kutoka Tanzania wiki hii

Kutoka kwa wasanii kama Zuchu, Hamadai, Rayvanny na wengineo wengi hizi hapa ni ngoma tano mpya kutoka Tanzania wiki hii:

Utaniua - Zuchu

Wiki hii Zuchu aliamua kuvunja ukimya kwa kuachia Utaniua, ngoma tamu ya mapenzi ambayo ndani yake Zuchu anahadithia jinsi penzi zito kutoka kwa mwenza wake linavyomchanganya. Ngoma hii ni maalum katika hiki cha wapendanao yaani Valentine

https://www.youtube.com/watch?v=e3erBs1myQo

Msela - Hamadai Ft Chid Beenz

Hamadai ni mwandishi mzuri sana  na karama hiyo amedhihirisha kwa mara nyingine kwenye Msela akiwa na Chid Beenz. Msela ni ngoma ambayo Hamadai anahadithia jinsi anavyopendwa na mtoto wa "kishua" kitu ambacho kinamfanya ashangae sana kwani yeye hana kitu.

https://www.youtube.com/watch?v=-BihOBgIPkM

Forever - Rayvanny

Wakati mashabiki wakiisubiri kwa hamu EP yake ya Flowers III, Rayvanny hivi karibuni ameachia Forever, ngoma nzuri ya mapenzi ambayo ndani yake Vanny anazungumzia jinsi ambavyo anapanga kuwa na mwenza wake milele yote.

https://www.youtube.com/watch?v=4E6imf1hZy4

Siwezi - Feza Kessy

Baada ya ukimya wa muda mrefu hatimaye Feza Kessy amerudi tena na ngoma mpya ya kuitwa Siwezi. Kwenye Siwezi, Feza Kessy anasema hapana kwa wanaume wanaomrubuni kwa vitu vidogo vidogo.

https://www.youtube.com/watch?v=JdlGmTjIAwo

 

 

Leave your comment