Harmonize Kuekeza Zaidi Ya 300M Video Mpya 

Picha Kutoka Instagram
Mwandishi:
Charles Maganga

Msanii anayeipeperusha vyema bendera ya Bongo Fleva duniani, Harmonize hivi karibuni amedokeza kwamba ametumia zaidi ya Milioni 300 kuandaa video ya muziki ambayo haijatoka. 

Harmonize ambaye kwa sasa anatamba na video yake ya “Zanzibar” ametoa taarifa hiyo hivi karibuni na hivyo kusababisha maoni mbalimbali kutoka kwa mashabiki zake na wadau mbalimbali wa muziki. 

Harmonize kwa sasa yuko nchini Marekani Miami kwa ajii ya ziara yake ya muziki na kupitia ukurasa wake wa Instagram, upande wa Instastory Harmonize aliweka video fupi inayomuonesha akiwa location na kudokeza kuwa kwa mara ya kwanza ametumia Dola 150,000 za kimarekani kuandaa video hiyo 

“My first time investing over 150k Usd Into A Music Video” aliandika Harmonize kwenye Instastory yake. 

Kwa mwaka 2023, Harmonize tayari ameshaachia video nne za muziki ambazo ni “Wote” “Best Friend” “Single Again” pamoja na “Zanzibar” ambayo imeongozwa na Director Kenny. 

Leave your comment