NGOMA MPYA - YANGA ANTHEM 2 Marioo Kwa Mashabiki wa Yanga


Imange courtesy Instagram
Mwandishi Charles Maganga

Msanii kutoka nchini Tanzania, Marioo kwa mara nyingine ameamua kuonesha mapenzi aliyonayo kwa klabu ya Yanga baada ya kuachia ngoma mpya kabisa ya kuitwa “Yanga Anthem 2” 

Yanga Anthem 2 inakuja siku chache tangu Marioo aachie toleo jipya la album yake ya “Yhe Kid You Know” ambayo ilikuwa na ongezeko la ngoma nne za moto ambazo ni “Tomorrow” “Sing” “Nikazama” na “Tunamjua” 

Kwenye “Yanga Anthem 2” Marioo anaonesha ni jinsi gani klabu ya Yanga inafanya huku akitumia maneno chokozi kuonesha namna gani Yanga “Inachambua wapinzani wao kama karanga”. Ngoma hii inetayarishwa na Kimambo Beats ambaye ni moja kati ya watayarishaji bora wa muziki kutoka Tanzania. 

Ikumbukwe kuwa hii ni ngoma ya pili kutoka kwa Marioo kuimbia klabu ya Yanga. Ngoma nyingine kutoka kwa Marioo  kuhusu Yanga inaitwa Yanga Anthem (Sisi Ndo Yanga) pamoja na Yanga Tamu ambayo ni remix ya wimbo wake wa Bia Tamu. 

Leave your comment