Nyimbo Mpya: Dulla Makabila 'Pita Huku', 'Dharau' Gigy Money na Ngoma Zingine Mpya Tanzania Wiki Hii

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Katika kipindi hiki ambacho tunaenda kufunga mwaka, wasanii mbalimbali wameendelea kuachia ngoma ambazo zimeendelea kufanya vizuri ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Zifuatazo ni ngoma mpya Tanzania wiki hii kutoka kwa wasanii kama Dulla Makabila, Gigy Money, Msodoki Young Killer na wengineo wengi.

Pita Huku - Dulla Makabila

Wiki hii Dullah Makabila aliachia ngoma yake ya kuitwa Pita Huku ambayo ndani yake alimulika watu wenye tabia mbalimbali ambazo hazifai kwenye jamii. Tangu kuachiwa kwake Pita huku imezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii huku watu wengi wakiwa wamemsifia Dullah Makabila kwa ubunifu wake.

https://www.youtube.com/watch?v=1aeVXLt5hOw

Sinaga Swaga Volume 6 - Msodoki Young Killer

Wakati albamu yake ya Msodoki Super Nyota ikiendelea kufanya vizuri, Msodoki aliamua kufunga mwaka kwa kuachia ngoma hii ya Sinaga Swaga Volume 6. Kama kawaida yake Young Killer amezungumzia kuhusu watu wasiompenda, kipaji chake kama msanii na mambo mengine mengi yanayohusu maisha.

https://www.youtube.com/watch?v=UwJscoFqwAc

Boss - Lukamba

Lukamba aliposema kwamba ameamua kuwa mwanamuziki alikuwa hata ii na ngoma yake ya Boss Imethibitisha kauli yake. Kwenye Boss Lukamba anatumia mdundo wa Amapiano kufikisha ujumbe kwa watu ambao wanaigiza maisha huku akisisitiza kwamba yeye kwa sasa ni Boss na ameshaachana na usela.

https://www.youtube.com/watch?v=tTX8NG8SPjg

Dharau - Gigy Money

Kwenye ngoma yake hii mpya ya kuitwa Dharau, Gigy Money ni kama anatuma salamu kwa mtu na ndani yake anasisitiza kwamba yeye hapendi Dharau. Dharau inakuja wiki chache tangu, Gigy Money aachie Saubona ambayo alimshirikisha Rosa Ree.

https://www.youtube.com/watch?v=gc1gSNSpLUw

Fashion Remix - Mtafya Featuring Nay Wa Mitego.

Kwenye ngoma hii Nay Wa Mitego anadokeza kuhusu vitu ambavyo wengi wanaviona ni vya kawaida yaani "Fashion" lakini kwa namna moja au nyingine haviko sawa. Hivi karibuni pia alishirkishwa na Kontawa kwenye Champion.

https://www.youtube.com/watch?v=UxjTuidcFLk

Leave your comment