Nyimbo Mpya: Mac Voice Ft Rayvanny 'Muongeze', Belle 9 'Watu' Na Ngoma Zingine Mpya Tanzania Wiki Hii

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Katika wiki hii ya kwanza kabisa ya kufungua mwaka zifahamu ngoma mpya kutoka kwa wasanii wa Tanzania ambazo sio tu kwamba zitakuburudisha lakini pia zitakupa mafunzo Ya kutosha.

Kutoka kwa wasanii kama Mac Voice, Rapcha na wengineo wengi, hizi ni nyimbo mpya Tanzania wiki hii :

Story Nyingine Freestyle - Rapcha

Katika wimbo huu Rapcha ameendelea kujigamba na kuonesha kuwa ana uwezo wa kipekee katika game ya Hip Hop nchini Tanzania. Huu ni wimbo ambao Rapcha anawakumbusha washindani wake wa kimuziki kuhusu kipaji chake na wengi kwenye mitandao ya kijamii wameuchukulia wimbo kama Diss Track.

https://www.youtube.com/watch?v=wpqcsk1XwFs

Watu - Belle 9

Belle 9 alinogesha kiwanda cha Bongo Fleva hivi karibuni na ngoma yake ya "Watu" ambayo inazungumzia kuhusu mapenzi na namna ambavyo baadhi ya watu wanajaribu kuangamiza mapenzi yake kwa mtu anayempenda.

https://www.youtube.com/watch?v=syNhCrrNiVc

 

Muongeze - Mac Voice Featuring Rayvanny

Baada ya "Tamu" Mac Voice pamoja na Rayvanny wamekuletea hii ya kuitwa "Tamu" ngoma ambayo ndani yake wasanii hawa wawili kutokea Next Level Music wanalenga kuburudisha watu ambao ni wahudhuriaji wazuri wa club na kumbi mbalimbali za starehe hapa Afrika Mashariki.

https://www.youtube.com/watch?v=1PZoWFI4Gq8

 

Hatia V - Dizasta Vina

Hata V ni wimbo ambao Dizasta Vina anasimulia na kueleza kuhusu maisha, mafunzo na ujasiri wa baba yake ambaye kwake yeye anamuona kama shujaa. Wengi wamesifia ngoma hii kutokana na ubunifu uliotumika kuelezea simulizi hii kutoka kwa Dizasta Vina.

https://www.youtube.com/watch?v=vdlnFatlP6Y

 

Dawa - Snow Wizzy

Moja ya wasanii chipukizi waliopamba wiki hii ni Snow Wizzy ambaye ametuletea ngoma yake ya kuitwa Dawa ambayo ndani yake anaeleza namna ambavyo anakoshwa na mwandani wake huku akitumia vionjo vya Afrobeats kufikisha ujumbe wake.

https://www.youtube.com/watch?v=as0z987ScqY

Leave your comment