Baba Levo Athibitisha Kumshirikisha Diamond Platnumz Kwenye Ep Yake

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Msanii kutoka Tanzania na mtangazaji wa Wasafi FM Baba Levo hivi karibuni amethibitisha kwamba amemshirikisha Diamond Platnumz kwenye EP yake.

Baba Levo ambaye alishawahi kuwa Diwani kabla ya kuingia kwenye utangazaji amethibitisha kuwa Simba ni moja ya wasanii ambao wapo kwenye EP yake anayotarajia kuiachia hivi karibuni. Baba Levo amekuwa akidokeza kwa muda mrefu sasa kuhusu ujio wa EP hiyo ambayo inaitwa 'Seven Wonders EP.'

Kwenye video ambayo inasambaa kwa kasi sana kwa sasa kwenye mitandao ya kijamii, Baba Levo alionekana akimsihi Diamond Platnumz kwamba asikilize ngoma yake mpya ambayo wamefanya pamoja kupitia zawadi ya Spika aliyompatia.

“Diamond Sikiliza ngoma yangu mpya aliyonisaidia aisikilizie humu” alisikika akisema Baba Levo kwenye video hiyo.

Ikumbukwe kuwa Diamond Platnumz na Baba Levo tayari wana ngoma ambayo inaitwa Shusha ambayo ilitoka mwaka 2021.

Leave your comment