Tommy Flavor Atangaza Kuachia Ngoma Mpya Na Marioo

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea lebo ya Kings Music, Tommy Flavour hivi karibuni ameingia kwenye Rada za vyombo vya habari Tanzania baada ya kutangaza ujio wa collabo yake na msanii nguli kutokea Tanzania, Marioo.

Tommy Flavor ambaye kwa muda mrefu sasa amekuwa akidokeza kuhusu ujio wa albamu yake ya kuitwa "The Heir To The Throne" ametoa taarifa hizo hivi karibuni ikiwa ni siku chache tu tangu aachie video yake ya Numero Uno ambayo amefanya na mwanamuzi kutokea nchini Kenya, Tanasha Donna.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Tommy Flavor amedokeza kuwa ngoma yake itaitwa Nakuja na atamshirikisha msanii Marioo na kuongeza kuwa ngoma hiyo itaachiwa mwezi Februari bila kutajwa maalum ambayo anatarajia kuachia kazi hiyo.

"Februari nakuja jamani na Marioo TZ, Niambie tarehe ngapi tuache hili goma?" alidokeza Tommy Flavor kwenye akaunti yake ya Instagram.

Wasanii wengine kutokea Tanzania wanaotarajia kuachia ngoma hivi karibuni ni pamoja na Ruby ambaye anatarajiwa kuachia ngoma na Otile Brown, Zuchu ambaye siku chache alidokeza ujio wake mpya pamoja na wasanii wengine kibao.

Leave your comment