Ngoma Kumi Kali Za Mapenzi Za Kusikiliza Kipindi Hiki Cha Valentine

[Picha: Screengrab/YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Kama kuna muda mzuri wa kumueleza mpenzi wako ni kwa namna gani basi kipindi hiki cha Valentine ndio muda mzuri zaidi na katika kufanikisha hilo, wasanii mbalimbali kutoka Tanzania wamekusaidia kueleza hisia zako kupitia ngoma hizi maalum za mapenzi.

Kutoka kwa wasanii kama Kusah, Diamond Platnumz, Jay Melody, Zuchu, Billnass na wengineo wengi, hizi hapa ni ngoma 10 kali za mapenzi kipindi hiki cha Valentine.

Nakupenda - Jay Melody.

Jay Melody anakusaidia kueleza hisia zako na jinsi ambavyo umedata kihisia kwa mpenzi kupitia Nakupenda. Hii ni ngoma maalum kwa siku kama ya leo ambapo wapendanao watakuwa wakielezana ya moyoni.

https://www.youtube.com/watch?v=LRdmZEdZ67g

 

Mi Amor - Marioo

Sauti ya Marioo na Jovial ziliweza kurandana vizuri kabisa katika juhudi zao za kueleza a ni kwa namna gani wapenzi wa atakuwa kupendana na kupeana furaha pindi wawapo pamoja na bila shaka kwa siku kama ya leo hii ni ngoma maalum kabisa kwa wapendanao.

https://www.youtube.com/watch?v=aU9Gmomi02Q

 

Hakuna Kulala - Zuchu

Hii ni ngoma ya kusikiliza usiku ukiwa faragha na mwenza wako katika siku hii ya Valentine. Kama utaiweka ngoma hii on repeat mara kwa mara utamsikia Zuchu akiwakumbusha kuwa hakuna kulala mpaka asubuhi iwakute.

https://www.youtube.com/watch?v=e50WOyUM160

 

Puuh - Billnass

Ukimuona mpenzi wako unajisikiaje? Raha, Furaha, Amani au na wewe moyo wako unadunda Puuh kama Billnass ambaye kwenye ngoma yake hii anamshukuru mpenzi wake kwa kumsikiliza na kumpenda pamoja na maneno hasi kwa watu kuwa mengi sana.

https://www.youtube.com/watch?v=G06aqtUnWt8

 

Forever - Rayvanny

Kwenye Forever Rayvanny, anamkumbusha mpenziwe kuwa watakuwa wote mpaka kifo na hii ni ngoma nzuri ya kuisikiliza iwapo utakuwa unataka kumuaminisha mwezi wako kuwa utakuwa nae milele na milele.

https://www.youtube.com/watch?v=4E6imf1hZy4

On Fire (Nakukunda) - Kusah

Kwenye Romantic EP ya kwake Kusah kuna ngoma hii ya kuitwa On Fire ambayo ndani yake kuna mashahiri mazuri kutoka kwa Kusah yanayofaa katika kipindi hiki cha Valentine. Mtumie ngoma hii umpendaye na utatushukuru baadae.

https://www.youtube.com/watch?v=pmzCDYIfwd4

Huyu Hapa - Mbosso

"Liwalo Na Liwe Leo Namtangaza" kama leo una mpango wa kufanya hafla fupi ili kumtambulisha mwenza wako kwa ndugu, jamii na marafiki basi "Huyu Hapa" ya Mbosso itakusaidia kufanikisha hilo.

https://www.youtube.com/watch?v=uidtFhrkC8s

Mtasubiri - Diamond Platnumz

Kwa wawili wanaopendana bila shaka ngoma hii ya Mtasubiri ya Diamond Platnumz na Zuchu haiwezi kuisha utamu masikioni mwao kutokana na mashahiri mazuri baina ya wawili hao.

https://www.youtube.com/watch?v=IokCG2J-_5Q

 

Fall In Love - Ruby

Ruby kwenye ngoma hii anaweka wazi ni kwa namna amezama mzima mzima kwenye himaya ya mpenzi wake na ni kupitia sauti yake tamu na mashahiri yake ya kusisimua utafahamu kwamba ngoma hii ni mahususi katika kipindi hiki cha Valentine.

https://www.youtube.com/watch?v=m92KMONCndE

Nakuja - Tommy Flavour Ft Marioo

Ukiweka kando kiitikio cha ngoma hii, utapenda namna ambavyo Tommy Flavour ameweza kuweka maneno mazuri ya mapenzi kuweza kumsifia mwandani wake.

https://www.youtube.com/watch?v=OJw3i72JEUc

Leave your comment