Harmonize, Country Boy Waachia Ngoma yao Mpya ‘Far Away’

[Anwani ya picha:Countrywizzy Instagram]

Mwandishi Branice Nafula

Tufuate Kwenye Google News

Wanamziki kutoka lebo ya Konde Music Worldwide Harmonize na Country Boy wameachia ngoma yao mpya kwa jina ‘Far Away’.

Hii ni mojawapo ya nyimbo sita kwenye ‘The Father’ EP ya Country Boy. Kupitia ngoma hii, wawili hao wanaendelea kudhihirisha ubabe wao kwenye mziki wa bongo.

‘Far away’ ni wimbo wa mapenzi ambapo Country Boy anaangazia namna mpenzi wake anavyomfurahisha.

Download Country Boy Music for Free on Mdundo

Wimbo huu unaangazia furaha ya kuwa na mpenzi anayekupenda bila matarajio mengi sana.

“Ushawai kupenda ila huwa ni too much, (too much), nahisi nachelewa mama call me back(call me back)anayajua mapenzi anasema mapenzi ndio yeye anajua kutega mitego , mitego ndio yeye, can you feel it baby…”

Harmonize kwa upande wake aliusuka wimbo huu kwa sauti na ubora wake.

Country Boy sasa ameachia ngoma zake zote sita kwenye hio EP mpya ‘The Father’.

Wenye hio EP amewashirikisha wasanii kutoka nchi ya Nigeria. Harmonize kuwepo kwenye hii EP itasaidia katika kumpatia Country Boy umaarufu zaidi katika sanaa yake ya mziki.

Huu ni wimbo wa pili wa ushirikiano kati ya Harmonize na Country Boy.

Kazi yao ya awali ni wimbo ‘Watoto’ kabla hajamtambulisha chini ya lebo ya Konde gang.

Kwa sasa wimbo huu unaendelea kupata umaarufu kwenye mtandao wa YouTube huku mashabiki wakingoja video rasmi.

 https://www.youtube.com/watch?v=7PhLgB5XYCQ&ab_channel=CountryWizzy

 

More News

Diamond Drops Another Big Song Dubbed ‘Haunisumbui’

Daev Biography, Music Career, Top Songs, Relationship, Net worth, Untimely Death and Much More

Late Zambian Musician Daev Shines on Mdundo Top 10 Weekly Chart

Eddy Kenzo Hits Out at Critics Linking his Music Success to Luck

Bobi Wine inspired me to Make it in Life - Mikie Wine

Jah Master Narrates How he Bounced Back to Music after Life’s Frustration

The Evolution of Gospel Music in Ghana

Sheebah, Crysto Panda’s 'Kyoyina Omanya' Remix Surpasses One Million Streams

Top Nigerian Albums/EPs Expected Before The End Of 2020

 

Leave your comment