Country Boy Kuzindua EP Yake Mpya ‘The Father’ Wikendi Hii

[Anwani ya picha:Countrywizzy Instagram]

Mwandishi Branice Nafula

Tufuate Kwenye Google News

Msanii wa Hip-hop kutoka lebo ya Kondegang Music World wide Country Boy ametangaza kuwa atafanya uzinduzi wa Ep yake mpya ‘The Father EP’ wikendi hii tarehe 25/09/2020.

Hii ni wiki mbili baada ya Country Boy maarufu kama Country Wizzy kuzinduliwa rasmi kama msanii mpya wa lebo hio inayoongozwa na Harmonize.

Katika taarifa ya uzinduzi kupitia ukurasa wake wa Instagram, Country Boy amewashukuru mashabiki kwa mapokezi mazuri wa nyimbo zake mbili ‘Intro’ na ‘Baba’.

Country Boy ameahidi show ya kushtukiza itakayofanyika mjini Masaki.

“Kwanza napenda kutoa shukrani zangu Kwa mapokezi mazuri na support kubwa ya kazi zangu! #Intro Na #Baba. Nafarijika sana na Mungu Awabariki sana. 25 SEPTEMBER 2020 Siku Ya Ijumaa Itakuwa Siku Rasmi Ya Ku Release #THEFATHEREP Na Party zima litafanyika Pale Mjini Masaki @Havoctanzania,” aliandika Wizzy.

Download Country Boy Music for Free on Mdundo

Ep yake Country Boy ina nyimbo sita. Tatu kati ya sita hizo ni ushirikiano na wasanii wengine kutoka Afrika Magharibi na mkuu wake Harmonize.

Kupitia ‘The Father’ EP, Country Boy anaonyesha umahiri na ustadi wake katika fani hii ya mziki wa Hip-hop Tanzania. Wanaotarajiwa Kuhudhuria shughuli hii ni wasanii wote katika lebo ya Konde Music World wide na wengineo.

 

More News

Diamond Drops Another Big Song Dubbed ‘Haunisumbui’

Daev Biography, Music Career, Top Songs, Relationship, Net worth, Untimely Death and Much More

Late Zambian Musician Daev Shines on Mdundo Top 10 Weekly Chart

Eddy Kenzo Hits Out at Critics Linking his Music Success to Luck

Bobi Wine inspired me to Make it in Life - Mikie Wine

Jah Master Narrates How he Bounced Back to Music after Life’s Frustration

The Evolution of Gospel Music in Ghana

Sheebah, Crysto Panda’s 'Kyoyina Omanya' Remix Surpasses One Million Streams

Top Nigerian Albums/EPs Expected Before The End Of 2020

 

Leave your comment