More songs by Download Best Latest Song Reviews/Analysis - Mdundo Podcast

Mwaka wa Elfu mbili Ishirini na tatu umekuwa wa kufana mno kwa wasanii wa Bongo huku wakijikakamua kutoa kibao baada ya kingine.

Japokuwa mwaka jana tulishuhudia wasanii wengi wakiachia albamu mpya za muziki kulinganisha na mwaka huu, wasanii hawa wa bongo bado wanatia jitihada kutupa vibao zaidi. Albumu za muziki ambazo zimeweza kutokea mwaka huu ni kama vile “Heir to the throne” yake Tommy Flavour, “Most People Want This” ya Navy Kenzo, “Flowers III” ya msanii Rayvanny na “Love Sentence” yake Lady Jay Dee miongoni mwa zinginezo. Katika sekta ya vibao, wanamuziki hawa wa bongo wametupa mchanganyiko wa nyimbo za mapenzi na nyimbo za kujiburudisha na kufurahia maisha. Sana sana tumeweza kushuhudia ushirikiano Kati yao wenyewe kwa wenyewe na ushirikiano mchache Kati Yao na wasanii wa nje kama vile Chley kutoka Afrika Kusini, Koffi Olomide na Innoss’ B kutoka Afrika Kati na Chike kutoka Afrika Magharibi.

Sifa moja inayojidhihirisha mno Kati ya nyimbo hizi ni ladha ya Amapiano ambayo imekuwa ikitumika mara kwa mara. Inazofuata ni orodha ya nyimbo kumi mpya ambazo zimetamba mwaka huu.
1.Enjoy kibao chake Jux anachomshirikisha msanii Diamond Platnumz
2.Sele kibao chake Mbosso akimshirikisha Chley
3.Nakuja wimbo wa Tommy flavour akimshirikisha Marioo
4.Nobody wimbo wake Darassa akimshirikisha Bien kutoka Kenya
5.My baby kibao chake Diamond Platnumz akimshirikisha Chike
6.wimbo Honey wa Mwanamuziki Zuchu
7.Nani kibao chake Zuchu na Innoss’ B
8.Sawa wimbo wake msanii Jay Melody
9.Achii ya Diamond na Koffi Olomide
10.Mahaba kibao chake Alikiba

Ijapokuwa hatujaweza kutaja vibao vyote vya mwaka huu unaweza kupata maelezo zaidi au chambuzi za nyimbo mpya za bongo katika tovuti ya www.mdundo.com.