• Stream Ali Kiba - Huku Feat. Tommy Flavour (Uchambuzi)

    Huku Feat. Tommy Flavour (Uchambuzi)

    Ali Kiba

    1:22

Hatimaye video tumekuwa tukiisubiria kwa hamu imetokea na ni yenye kuchochea hisia njema mno.

Iwapo hujui naongelea nini bado namaanisha video mpya ya wimbo huku wa Alikiba ambao amemshirikisha Mwanamuziki Tommy Flavor. Huku ni wimbo mtamu ulio na mada ya mapenzi na kwa kuchanganya sauti zao nyororo na tulivu, wasanii hawa wanaimba kwa mvuto katika wimbo huu na kuufanya wa kufana mno.

Mdundo wake umechanganya ladha ya Amapiano na Bongo Flava ambao humvutia mtu kutaka kusimama na kudensi. Kanda ya video vile vile inafuata mkondo huo na ni ya kuvutia haswa kwa vijana Kwani inaonyesha densi za kusisimua na kuonyesha maisha ya vijana wa siku hizi ya anasa na raha. Densi hizi zinaeza igwa na vijana sana sana kwenye mtandao wa kijamii wa TikTok.

Ki ukweli wimbo huu ni wa kuburudisha mno na unaweza kusikilizwa mno Kwani ubunifu wake na Sanaa ya utunzi wa wimbo huu unaweza kumfanya mtu kuwa na mazoea ya kuusikiliza. Kupata taarifa za nyimbo zinazotamba barani Afrika tembelea tovuti ya www.mdundo.com.