• Stream Ali Kiba - Alikiba - Mahaba (Official Audio) Review

    Alikiba - Mahaba (Official Audio) Review

    Ali Kiba

    1:27

Lyrics

Alikiba - Mahaba

Mkurungenzi Mkuu wa Lebo ya Kings Music Alikiba ameachia kazi mpya kwa jina ‘Mahaba’. Mwimbaji huyo amewafurahisha mashabiki kwa kkazi hii waliokuwa wamesubiria kazi yake ya kwanza mwaka huu 2023.

Wimbo huu unaambatana na maudhui ya mwezi huu wa mapenzi ambapo watu kote ulimwenguni walipata fursa ya kuwa na wapenzi wao siku ya Valentine ambayo huwa tarehe 14 Februari.
View more

Mdundo.co is home to alikiba mahaba audio get to know about alikiba wife and download free alikiba songs download mdundo

Lyrics

Siku hizi hakuna mahaba
Yeah, mahaba
Mapenzi ya mkataba
Mpaka kufa, yamekwisha

Ni neema ukiwa unahema
Mapenzi yanachosha, yanafuja raha
Nafsi yangu inasema
Bora nimpende tu alionizaa

Uchungu wa kulia daily
Mapenzi yalinifanya nisile
Sina kumbukumbu ile
Kwamba ulinikosha, no!

Uchungu wa kulia daily
Mapenzi yalinifanya nisile
Sina kumbukumbu ile
Yakwamba ulinikosha, no!

Mwenzako mi' nilikufa, nikazikwa, nikaoza
Mapenzi yalinitesa, yalinitupa, nimefufuka, yeah
Mi' nilikufa, nikazikwa, nikaoza
Mapenzi yalinitesa, nimefufuka, yeah

S'kiza kwanza we dada
We dada
Mi' sio mgeni alishanikaba
Mapenzi yalinikausha

Natamani kuwa single
Ila nna-upwilu unakaba koo
Mabinti wenye vifundo
Hao ndio mi' wananitoa roho

Na siri juu ya jambo lile
Ni kama chakula lazima nile
Mi' mbovu sana wa jambo lile
Na ufundi wa kutosha, ooh

Na siri yake tuu jambo lile
Ni kama chakula lazima nile
Mi' mbovu sana wa jambo lile
Na ufundi wa kutosha, ooh

Mwenzako mi' nilikufa, nikazikwa, nikaoza
Mapenzi yalinitesa, yalinitupa, nimefufuka, yeah
Mi' nilikufa, nikazikwa, nikaoza
Mapenzi yalinitesa, nimefufuka, yeah