Msanii wa muziki wa kufoka kutokea Tanzania anayefahamika kama Nay wa Mitego au Nay true boy ameachia kibao kipya kinachojulikana kama Mamlaka. Mamlaka ni wimbo ambao una ladha ya muziki wa bongo ambao huanza kwa mdundo mtulivu ulio na lahani ya piano. Kwa talanta na ubunifu wake, Msanii huyu anautunga wimbo unaohakiki serikali na viongozi ambao wamezama katika limbwi la cheo na uongozi na kusahau kuzingatia maslahi ya wananchi waliowachagua.

Katika wimbo huu, Msanii anaomba siku moja tu watu wa kawaida au walio na vyeo vya chini wangeweza kufurahia maisha ambayo wabunge wanaishi. Kunukuu maneno ya wimbo huu, mtunzi anaaomba kuwa angekuwa Rais wa Nchi ya Tanzania ili kuwe na siku ya Mamlaka ambayo wananchi wote wangepata maisha ya nafuu ilhali wabunge wanateseka, Walimu na Askari watapate mishahara ya wabunge kisha wabunge wapate mshahara wa chini. Msanii Nay wa mitego anaamua kuwa mwanaharakati wa kijamii Kupitia utunzi wake ili kuwatetea wanyonge na wanaonyanyaswa katika Jamii na matendo ya kibinafsi ya viongozi ambao hawaweki ahadi zao kwa wailowachagua.

Wimbo huu unafaa Kwani unaadhari nzuri katika jamii na unawakosoa viongozi na kuwakumbusha wazingatie maslahi ya wanainchi.

Kupata chambuzi za muziki na habari za nyimbo mpya barani Afrika tembelea tovuti ya Mdundo.com.