Nay Wa Mitego Aachia Ngoma Mpya "Kudadadeki"
10 March 2023
[Picha: Instagram]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram
Kutoka kwenye tasnia ya Hip Hop nchini Tanzania, rapa Nay Wa Mitego amerudi tena na mkwaju wake mpya kabisa wa kuitwa Kudadadeki.
Kabla ya ngoma hii, wiki 3 zilizopita Nay Wa Mitego aliachia ngoma "We Don't Care" ambayo amemshirikisha Mr Blue na hivyo kufanya ngoma hii ya Kudadadeki kuwa ngoma yake ya tatu kwa mwaka huu wa 2023.
Kama kawaida yake, kwenye Kudadadeki, Nay Wa Mitego anatoa mafunzo na kuzungumzia yale ambayo yanaendelea kwenye jamii kwa sasa. Kwenye ngoma hii Nay Wa Mitego amegusia kuhusu elimu, maisha ya mtaani, ukosefu wa uaminifu kwenye mahusiano na mengineyo mengi.
Leave your comment