Nay Wa Mitego Akosoa Tuzo Za Muziki Tanzania

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Msanii kutoka Tanzania, Nay Wa Mitego hivi karibuni amekosoa waandaaji wa tuzo za Tanzania Music Awards ambazo huandaliwa na Baraza La Sanaa Tanzania, BASATA.

Hivi karibuni BASATA walitangaza orodha ya wanamuziki wanaowania tuzo za muziki Tanzania ambapo katika orodha hiyo wasanii kama Zuchu, Harmonize, Ali Kiba, Marioo walitajwa kuwania vipengele mbalimbali.

Kwa upande wa Nay Wa Mitego wimbo wake wa “Seketula” ambao amemshirikisha Runtown wa Nigeria ulitajwa kwenye kipengele cha collabo bora ya kimataifa.

Akizungumza hivi karibuni kwenye mahojiano na kituo cha redio hapa Tanzania, Nay Wa Mitego alidokeza kuwa hajapendezwa na kitendo cha BASATA kuweka wimbo wake kwenye tuzo hizo kwani tangu mwanzo alitangaza kutoshiriki kwenye tuzo hizo na ndio maana hakupeleka kazi zake kwa waandaaji wa tuzo hizo.

“Sijawahi ku-submit mimi kushiriki kwenye tuzo zao lakini wameweka wimbo wangu kwenye category lakini mimi nilishawahi kusema sitawahi kushiriki kwenye tuzo zozote zinazoandaliwa na kitu kinaitwa BASATA. Wame-submit wimbo wangu wa Seketula ambao nimemshirikisha Runtown kiukweli kabisa sijapenda” alizungumza msanii huyo.

Wasanii wengine waliojitokeza kukosoa tuzo hizo ni pamoja na Mbosso, Rayvanny, Baba Levo, Moni Centrozone, Baraka The Prince na wengineo wengi”https://www.youtube.com/watch?v=NeFoZtpB1KM

Leave your comment