Nay Wa Mitego Aachia Rasmi Albamu Yake Ya "Rais Wa Kitaa"

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Mwanamuziki na rapa kutokea nchini Tanzania Nay Wa Mitego kwa mara nyingine amekonga hisia za mashabiki zake baada ya kuachia rasmi albamu yake ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu sana na mashabiki ya kuitwa "Rais Wa Kitaa".

Albamu ya Rais Wa Kitaa inakuja siku chache tangu rapa huyo adokeze kuhusu ujio wa albamu hiyo ambayo ni ya kwanza kutoka kwake tangu aingie kwenye tasnia ya muziki zaidi ya miaka 10 iliyopita.

Albamu ya Rais Wa Kitaa imesheheni ngoma 14 za moto huku wasanii mbalimbali kutoka Tanzania kama AY Master, Marioo, Ali Kiba, Maua Sama, Jux na One Six huku wasanii wengine wa kimataifa kama Runtown kutoka Nigeria pamoja na Kelechi Africana kutoka Kenya wakiwa wameshirikishwa kwenye albamu hiyo.

[Picha: Instagram]

Katika albamu hii Nay Wa Mitego ameshirikiana na watayarishaji tofauti tofauti wa muziki kutoka Tanzania ikiwemo Gachi B, Yogo Beats, Truename, Lollipop, Mr Lg, Mr T Touch pamoja na Chibby Beats.

Albamu hii inakuja katika kipindi ambacho Nay Wa Mitego anapata utambuzi wa kimataifa ambapo hivi karibuni msanii huyo alitajwa kuwania vipengele viwili kwenye tuzo za Zikomo za huko nchini Zambia na pia kwenye tuzo za Afrimma ametajwa kuwania vipengele viwili ikiwemo cha Rapa Bora wa Afrika.

Leave your comment