Nay Wa Mitego Azungumzia Kuhusu Tozo Kwenye Ngoma Yake Mpya 'Sauti Ya Watu'

Download FREE Mp3 Music by Nay Wa Mitego

Rapa kutokea nchini Tanzania Nay Wa Mitego kwa mara nyingine ameonekana kuguswa na hali inayoendelea nchini Tanzania kwa kuachia ngoma yake mpya kabisa ya kuitwa Sauti Ya Watu. 

Nay Wa Mitego ambaye wiki chache zilizopita alitangazwa kuwania kipengele kwenye tuzo kubwa za Afrimma ameachia mkwaju wake mpya wa Sauti Ya Watu ambao unakuja takriban mwezi mmoja tangu rapa huyo aachie albamu yake ya Rais Wa Kitaa. 

Kabla ya kuachia Sauti Ya Watu, Nay Wa Mitego alikuwa amejikita kuimba ngoma za mapenzi na ngoma hii inatukumbusha ngoma zake za zamani ambazo zilimpa umaarufu mkubwa sana. 

Kwenye Sauti Ya Watu Nay Wa Mitego anazungumzia mambo ambayo yanaendelea nchini Tanzania kwa sasa ikiwemo hali ya kisiasa ilivyo, uendeshwaji wa serikali, mdororo wa kiuchumi, ukosefu wa ajira na mambo mengine mengi. 

Ngoma hii imesindikizwa na video kali ambayo inamuonesha Nay Wa Mitego akiwa amefungwa kwenye minyororo huku akiwa amezungukwa na watu ambao hawatoi msaada wowote kisha baadaye anaonekana akiwa anachimba shimo balo baadae anaonekana akiwa anafukiwa. 

Leave your comment