Dayna Nyange Aeleza Mbona Hakuachia Video ya ‘Nitulize’ Aliyomshirikisha Nay Wa Mitego

[Picha: Dyana Nyange Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki wa Tanzania Dayna Nyange kwa mara ya kwanza amefunguka kwanini hakuachia video ya wimbo wake wa ‘Nitulize’ ambao alimshirikisha Nay Wa Mitego.

Wimbo huo ambao ulitolewa miaka michache zilizopita ulienea kwenye wavuti na ukagonga vichwa vya habari.

Soma Pia: Dayna Nyange Aeleza Kwanini Anataka Kupenya Soko la Muziki Nchini Nigeria

Dayna Nyange wakati huo alikuwa maarufu na karibu kila kituo cha habari kilitaka kufanya mahojiano naye. Mwanamuziki huyo, hata hivyo, alisusia mahojiano na majadiliano yoyote ambayo yalikuwa yanahusiana na wimbo wa ‘Nitulize’.

Kulingana na Dayna Nyange, alikuwa na uoga mwingi wakati huo na hakutaka  ngoma ile iwe kubwa kwa kuwa alikuwa amechoshwa na simu kutoka kwa wanahabari na mashabiki.

“Nilipoachia cover, kila mtu Dyana akaachia cover na Nay wa Mitego, nkikaa hivi naona watu wamenipigia…Nlikuwa na uoga, ni mazingira ambayo sijaizoea,” alisema Dyana.

Soma Pia: Dayna Nyange Afunguka Jinsi Alivyomshawishi Davido Kufanya Collabo Naye

Kwa sasa Dayna Nyange ni msanii anayevuma Tanzania baada ya kuachia wimbo wake ‘Elo’ akimshirikisha Davdo wa Nigeria.

Akizungumza na wahabari hivi majuzi, Dayna alisema kuwa wasimamizi wake ndio waliofanikisha kazi ile na Davido.

"Ni management ambayo nimefanya nayo kazi kwa muda mrefu. Ata ukiangalia wimbo wangu was Salama utaona kuna 3rd base media. So management ya muda mrefu," Dayna alisema.

 Kulingana na Dayna, ni ngumu kwa mwanamuziki wa Tanzania kupenya kwenye tasnia ya burudani ya Nigeria. Kwa hivyo, alikuwa na furaha kwamba wimbo wake ulikuwa umefanya vizuri licha ya kwamba ilikuwa mradi wake wa kwanza Afrika Magharibi.

Dayna ni mmoja wa wanamuziki wanaokua kwa kasi katika tasnia ya burudani ya Tanzania.

Leave your comment