Dayna Nyange Afunguka Jinsi Alivyomshawishi Davido Kufanya Collabo Naye
10 June 2021
[Picha: Dyana Nyange Instagram]
Mwandishi: Brian Sikulu
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Mwanamuziki wa Tanzania Dayna Nyange amejitokeza kueleza jinsi alivyofanya kazi na mwanamuziki wa Nigeria Davido.
Dayna alishangaza wengi wakati aliachia wimbo pamoja na Davido. Ukweli kwamba Dayna ni mwanamuziki anayekuja na Davido tayari anavuma Afrika na dunia nzima ndio iliyoufanya wimbo huo kuwa maarufu zaidi.
Soma Pia: Nyimbo Mpya: Zuchu, Diamond, Alikiba na Wasanii Wengine Wanoatarajiwa Kuachia Ngoma Mpya
Wimbo huo uliopewa jina la 'Elo' ulipokelewa vyema na mashabiki wake na kumfanya Dayna apate umaarufu zaidi.
Swali kubwa ni jinsi gani Dayna aliweza kumshawishi Davido afanye kazi naye. Katika mahojiano ya hivi karibuni, Dayna alielezea kuwa alitambulishwa kwa Davido na menejimenti yake ambayo kwa kiasi kikubwa iko nchini Nigeria.
Soma Pia: Zuchu Nyimbo Mpya: Ngoma Tano Zilizomfanya Zuchu Kuwa Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki
Dayna alielezea kuwa amekuwa akifanya kazi chini ya usimamizi ambao unajulikana kama 3rd Base Media kwa muda mrefu sana. Alisisitiza kuwa ushirikiano huo ulikuwa na mafanikio kwa sababu ya usimamizi wake.
"Ni management ambayo nimefanya nayo kazi kwa muda mrefu. Ata ukiangalia wimbo wangu was Salama utaona kuna 3rd base media. So mismanagement ya muda mrefu," Dayna alisema.
Kulingana na Dayna, ni ngumu kwa mwanamuziki wa Tanzania kupenya kwenye tasnia ya burudani ya Nigeria. Kwa hivyo, alikuwa na furaha kwamba wimbo wake ulikuwa umefanya vizuri licha ya kwamba ilikuwa mradi wake wa kwanza Afrika Magharibi.
Dayna ni mmoja wa wanamuziki wanaokua kwa kasi katika tasnia ya burudani ya Tanzania.
Leave your comment