Zuchu Nyimbo Mpya: Ngoma Tano Zilizomfanya Zuchu Kuwa Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki

[Picha: Zuchu Instagram]

Mwandishi: Omondi Otieno

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Zuchu ni moja wapo wa wasanii wanaotamba Afrika Mashariki licha ya kuwa na uzoefu wa mwaka moja pekee kwenye tasnia ya muziki.

Zuchu amepata umaarufu mkubwa kutokana na muziki wake wa hali ya juu na inayopendwa na wengi.

Kwenye nakala hii, tunaangazia ngoma tano zilizomskuma Zuchu kuwa msani bora wa kike Afrika Mashariki:

Sukari - Zuchu

Huu ulikua wimbo wake wa kwanza mwaka huu ambapo zuchu anazungumzia utamu ulio kwenye mapenzi. Kufikia sasa una watazamaji zaidi ya milioni thelathini na nane.

Soma Pia: Wasifu wa Zuchu, Nyimbo Zake Bora, Tuzo Alizoshinda, Mahusiano na Thamani Yake

https://www.youtube.com/watch?v=CCmItvVgn6Q

Litawachoma

Katika wimbo huu, Zuchu amemshirikisha Diamond Platnumz. Hii ilikua moja ya nyimbo mbili zilizochiwa mara moja ndani ya wasafi. Litawachoma iliangazia chuki za watu kuhusu mapenzi yake Zuchu na mpenziwe. Kufikia sasa ngoma hii inawatazamaji zaidi ya milioni kumi na tano kwenye YouTube.

Soma Pia: Mafanikio 5 Kuu ya Zuchu Mwaka Mmoja Baada ya Kuzinduliwa na WCB

https://www.youtube.com/watch?v=g9spgkHS2bs&ab_channel=Zuchu

 

Nobody  

Kwenye Nobody, Zuchu amemshirikisha Joeboy. Huu ni wimbo wake wa kwanza kushirikiana na msanii wa kimataifa. Nobody ilimpa Zuchu fursa ya kuimba lugha ya Kiswahili na Kiingereza ili kufikia soko hilo la magharibi.

https://www.youtube.com/watch?v=04Roh3SDyN0&ab_channel=ZuchuZuchuOfficialArtistChannel

Nisamehe

Huu ni wimbo kutoka EP yake ya ‘I am Zuchu’ iliyopokelewa kwa ukubwa na mashabiki wa Tanzania. Huu ni wimbo unaongazia uchungu wa kumuona mpenzi wako wa zamani akiingia kwenye ndoa. Ni wimbo ulio na watazamaji zaidi ya millioni Kumi.

https://www.youtube.com/watch?v=-Ze28ZMQlH4&ab_channel=ZuchuZuchuOfficialArtistChannel

 

Cheche

Zuchu amemshirikisha Diamond Platnumz kwenye wimbo huu. ‘Cheche’ ni wimbo wenye mdundo wa kizomba na kitaliano ambao ulimpa Zuchu sifa hadi nchi za kimataifa kwa ufundi wake katika sanaa. ‘Cheche’ ni wimbo wa upendo na furaha. Kwa sasa ni wimbo ulio na watazamaji zaidi ya milioni ishirini.

https://www.youtube.com/watch?v=vyUslddxOpI&ab_channel=ZuchuZuchuOfficialArtistChannel

 

Leave your comment