Wasifu wa Zuchu, Nyimbo Zake Bora, Tuzo Alizoshinda, Mahusiano na Thamani Yake

[Picha: Zuchu Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Zuchu ni nani na ana miaka mingapi?

Jina la usani: Zuchu

Jina Halisi: Zuhura Kopa

Tarehe ya kuzaliwa: 22 Novemba 1993 (miaka 28)

Aina ya mziki: Bongo Fleva, Baibuda

Thamani ya jumla: haijulikani

Soma Pia: Nyimbo Mpya 5 Zinazovuma Bongo Wiki Hii [Video]

Maisha ya mapema ya Zuchu yalikuwaje?

Zuhura Kopa ni mzaliwa wa Zanzibar na ni binti wa mwimbaji nguli wa Taarab Bi Khadija Omar Kopa. Zuchu alilelewa katika familia ya muziki ambapo aliapata tamaa ya kufanya mziki. Maisha yake kwa wingi amekua mji wa Zanzibar na hata masomo yake. Kisha baadae alienda India kusomea kozi za biashara kama msanii wa mziki wa kizazi kipya.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Diamond, Mbosso Waachia Video ya Ngoma Yao 'Baikoko'

Zuchu alianzaje kazi yake ya muziki na lini?

Zuchu alijitokeza kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wa muziki mnamo 2015 baada ya kushiriki kwenye mashindano ya Tecno Take The Stage ambayo yalifanyika nchini Nigeria. Licha ya kutoshinda mashindano hayo, Zuchu hakuacha ndoto yake ya muziki.  Alijitosa kwenye uwanja wa kufanya muziki wa wasanii wengine na kutoa nyimbo hizo baadhi zikiwa za waimbaji wa Wasafi haswa za Mbosso.

Kabla ya kuzinduliwa rasmi na Wasafi, alikuwa kwenye makao ya WCB kwa miaka minne, akiandaa ufundi wake vizuri na hata kuandika nyimbo zake mwenyewe. Zuchu alizinduliwa rasmi na Wasafi mnamo Machi 2020 na mwaka mmoja baadae Zuchu anajipigia upatu wa kazi zake na umaarufu aliopata.

Je, Zuchu ana Albamu?

Kufikia sasa Zuchu hana albamu, lakini ana EP inayoitwa 'I am Zuchu'. EP hio ina nyimbo saba ambazo ni;

 • Wana
 • Kwaru
 • Mauzauza
 • Raha
 • Nisamehe
 • Ashua
 • Hakuna Kulala

Mbali na nyimbo hizo, Zuchu ana nyimbo zingine na collabo kama vile:

 • Litawachoma ft Diamond Platnumz
 • Cheche ft Diamond Platnumz
 • Nobody ft Joeboy
 • Number One – Rayvanny ft Zuchu
 • Sukari

Zuchu ameshinda tuzo ngapi?

Chini lebo ya WCB, Zuchu ameweza kuteuliwa kwenye tuzo mbali mbali na kushinda kadhaa kama vile tuzo la Afrimma la msanii mpya barani Afrika, pia alijaribu kusukumia kuwa katika tuzo za Grammy lakini hakufanikiwa.

Mahusiano ya Zuchu

Zuchu ameweza kuweka maisha yake ya kibinafsi kibinafsi. Walakini hivi karibuni katika mahojiano Zuchu alithibitisha kuwa yeye hachumbiani na mtu yeyote.

Thamani Halisi

Kuhusu thamani yake halisi, haijulikani ni kiasi gani ana thamani, kwani hajajadili suala hilo.

https://www.youtube.com/watch?v=CCmItvVgn6Q

Leave your comment