Nyimbo Mpya: Diamond, Mbosso Waachia Video ya Ngoma Yao 'Baikoko'

[Picha: Diamond na Mbosso Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii wa WCB Mbosso ameachia kanda ya wimbo wake ‘Baikoko’ ambapo alimshirikisha bosi wake Diamond Platnumz.

‘Baikoko’ ni mojawapo ya nyimbo kutoka albamu ya Mbosso ‘Definition of Love’ alioiachia mwezi machi 2021.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma 5 Kali Kutoka WCB Mwaka wa 2021

Video hii inakua ya pili kutoka wa albamu hiyo baada ya ‘Yalah’ iliotoka wiki chache zilizopita.

‘Definition of Love’ ilipokewa kwa kishindo huku wimbo huu wa ‘Baikoko’ ukivuma zaidi haswa nchini Tanzania na Kenya.

‘Baikoko’ ni wimbo wa kumsifia dada mmoja anayewapendeza waimbaji hawa kwa maumbile yake na minenguo.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Nyimbo 10 Bora Kutoka Bongo Zilizoachiwa Machi 2021 [Video]

Mbosso anaanza wimbo huu kwa kumsifu binti huyo huku akieleza anavyompagawaisha.

“Eeeh, kako fine Kila nikitaka kwenye line, (bila bila) Shuwine, kwake nimelewa kama wine (tilalila) Ye sisimizi nami gegedu tunagegeduana (gege) Na nilivyo sina jinsi Tajiri wa mbegu namuonga na mwana…” aliimba Mbosso.

Katika mistari yao, Mbosso na Diamond Platnumz wametumia ufundi mkubwa kishairi kupasha ujumbe wao. Vile vile kanda ya wimbo huu ilifanyiwa kazi nzuri kuanzia kwa mavazi ya kimitindo na densi ikiongozwa na msakataji maarufu wa Wasafi Angel Nyigu.

Kufikia sasa ni wimbo unaokuwa kwa kasi katika mtandao wa YouTube na imefikisha watazamji zaidi ya elfi tisini chini ya masaa mawili. Video hii ilifanyiwa uelekezaji na director Kenny wa Wasafi .

https://www.youtube.com/watch?v=hGqzvvbZnyQ

Leave your comment