Nyimbo Mpya: Ngoma 5 Kali Kutoka WCB Mwaka wa 2021

[Picha: Zuchu Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Wasafi Classic Baby (WCB) ndio lebo maarufu sana nchini Tanzania haswa katika muziki. Lebo hii inayomilikiwa na msanii maarufu Diamond Platnumz imeweza kuwapa wasanii wengine fursa ya kujikimu. Katika nakala hii tunaangazia nyimbo tano bora kutoka WCB mwaka huu 2021:

Sukari - Zuchu

Huu ulikua wimbo wake wa kwanza mwaka huu ambapo zuchu anazungumzia utamu ulio kwenye mapenzi. Kufikia sasa una watazamaji zaidi ya milioni ishirini na tatu.

Soma Pia: Pakua Mixtapes Tano Kali za Hip Hop Kutoka Bongo kwenye Mdundo

https://www.youtube.com/watch?v=CCmItvVgn6Q

Kiuno - Rayvanny

Hii ilikuwa video yake ya kwanza mwaka huu katika lebo ya wasafi. Rayvanny anasifia mauno ya mpenzi wake .Kufikia sasa ni wimbo ulio na watazamaji zaidi ya milioni nne.

https://www.youtube.com/watch?v=r573wpRMtaA

Baikoko - Mbosso ft Diamond Platnumz

Hii ni mojawapo ya wimbo kutoka katika albamu yake mpya “Definition of Love”. Baikoko ni wimbo unaoshabikiwa sana licha ya kutokuwa na video yake. Kufikia sasa wimbo huu una watazamaji zaidi ya milioni moja.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Nyimbo 10 Bora Kutoka Bongo Zilizoachiwa Machi 2021 [Video]

https://www.youtube.com/watch?v=O7YvjudnAuk

Wale Wale - Lava lava

Wale Wale ni video ya kwanza kutoka kwenye EP ya Lava Lava kwa jina ‘Promise’ alioachia mwezi Februari. Wale wale inaelezea uchungu ambao hujitokeza katika uhusiano watu wakianza usaliti.

https://www.youtube.com/watch?v=gPrPHvmrC0U

Yalah - Mbosso

Huu ni wimbo pia kutoka kwenye albamu ya Mbosso na ndio video ya kwanza humo. Mbosso anaelezea uwezekano wa upendo kati ya watu wawili wenye maisha na hadhi tofauti.

https://www.youtube.com/watch?v=ijm4CHvJdGw

 

Leave your comment