Nyimbo Mpya 5 Zinazovuma Bongo Wiki Hii [Video]

[Picha:Fotojet/Prof/Jux/Mbosso/Diamond]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Baada ya siku za maombolezo kukamilika nchini Tanzania kufuatia kifo cha aliyekuwa rais wa nchi hiyo hayati Dkt. John Pombe Magufuli, wasanii wamerudi studioni na kuachia kazi nzuri wiki hii.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Diamond, Mbosso Waachia Video ya Ngoma Yao 'Baikoko'

Katika nakala hii, tunaangazia nyimbo tano mpya zinazovuma bongo wiki hii:

Lala - Rayvanny ft Juma Jux

Lala’ ni wimbo ambao wasanii hao waangazia kumzimia binti mmoja ambaye kwenye kanda hii ni mtayarishaji wa video za mziki. Pia wanawachezea shobo wapenzi wao wa awali Vanessa Mdee na Fayvanny.

https://www.youtube.com/watch?v=s3kdjHUPlXA

Baikoko - Mbosso ft Diamond Platnumz

Hili ndio toleo jipya kutoka kwa mastaa hawa wawili wanaosifia mpenzi wao. ‘Baikoko’ ni wimbo wa densi unaolezea maana ya kipekee ya mapenzi. Wimbo huu unaendelea kupata umaarufu kwa kasi sana.

https://www.youtube.com/watch?v=hGqzvvbZnyQ

Utaniambia Nini - Prof Jay

Utaniambia Nini’ ni kazi yake ya kwanza tangu kurejea katika ulingo wa mziki baada ya miaka mitano kama mbunge wa Mikumi.Katika wimbo huu anakashifu majifu ya wanamzii wa kisasa. Kufikia sasa ni wimbo ulio na watazamaii zaidi ya laki moja.

Soma Zaidi: Nyimbo Mpya: Diamond, Mbosso Waachia Video ya Ngoma Yao 'Baikoko'

https://www.youtube.com/watch?v=I2WN49sqQS4

For You - Marioo

Katika wimbo huu Marioo anashangaa ni vipi hakujua uzuri ulio kwenye mapenzi. Katika mistari yake anasema amejua kuwa hii dunia ni tamu kwa sababu ya mapenzi.Kufikia sasa wimbo huu una watazamaji zaidi ya laki moja.

https://www.youtube.com/watch?v=e3Aym00lfB4

Mapenzi - Ibraah

Katika wimbo huu, Ibraah anaangazia uchungu ulio kwenye uhusiano ya mapenzi. Ibraah anasema kuwa katika maisha binadamu anaweza vumilia vitu vingi ila tu si mapenzi.Kwa sasa ni wimbo unaoendelea kupata umaarufu na watazamaji zaidi ya laki mbili.

https://www.youtube.com/watch?v=q_0A3pvSehs

Leave your comment