Mafanikio 5 Kuu ya Zuchu Mwaka Mmoja Baada ya Kuzinduliwa na WCB

[Picha: Zuchu Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika kutoka lebo ya WCB Zuchu anasherekea mwaka mmoja baada ya kuzinduliwa kama msanii rasmi.

Ndani ya miezi kumi na miwili iliypita, Zuchu amepata umaarufu mkubwa zaidi kuliko msanii yeyote katika bara la Afrika Mashariki.

Hivyo katika nakala hii, tunaangazia mafaniko yake thabiti katika mziki ndani ya mwaka mmoja kama msanii:

Ridhaa (Endorsments)

Mwaka mmoja baadae Zuchu anajisifia kwa kupata ridhaa kadhaa ya makampuni tajika nchini humo. Kwa sasa Zuchu anafanya kazi na kampuni ya nywele ya Darling Tanzania, Tridea Cosmetics ya mafuta ya kujipaka na vilevile akapewa ubalozi wa kuendeleza utalii wa kisiwa cha Zanzibar.

Utazamaji na usajili kwenye YouTube

Zuchu ameweka rekodi mbali mbali na nyimbo zake. Kufikia sasa, Zuchu ndio msanii wa kwanza wa kike kutoka Afrika mashariki aliye na watazamaji zaidi ya milioni mia moja arobaini na nane na ana wasajili zaidi milioni moja kwenye chaneli yake ya YouTube.

Soma Pia: Nyimbo Mpya 5 Zinazovuma Bongo Wiki Hii [Video]

Kuteuliwa kwa tuzo mbali mbali

Chini lebo ya WCB, Zuchu ameweza kuteuliwa kwenye tuzo mbali mbali ndani ya mwaka mmoja. Vile vile Zuchu alipata nafasi ya kutueliwa kwenye Afrimma awards na kushinda taji la msanii mpya barani Afrika, pia alijaribu kusukumia kuwa katika tuzo za Grammy lakini hakufanikiwa.

Ushirikiano na wanamuziki tajika

Kwa muda huu mfupi Zuchu pia alipata kufanya nyimbo za ushirikiano na wasanii mbali mbali kama vile Diamond Platnumz, Rayvanny, Mbosso na kutoka nchini Nigeria alifanya wimbo wa ‘Nobody’ na Joeboy.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma 5 Kali Kutoka WCB Mwaka wa 2021

Kuachia Nyimbo Moto Zikifwatana

Baada ya kuzinduliwa, Zuchu aliapa kuachia mziki kwa ukaribu. Hivyo, Zuchu amekua katika harakati za kuachia mziki bila ya kukaa kwa muda mrefu. Hii ikiwa sababu ya kuongeza umaarufu wake kwa mashabiki zake.Kwa sasa Zuchu anatamba na wimbo wake ‘Sukari’.

https://www.youtube.com/watch?v=CCmItvVgn6Q

Leave your comment