Dayna Nyange Aeleza Kwanini Anataka Kupenya Soko la Muziki Nchini Nigeria

[Picha: Dyana Nyange Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki wa Tanzania Dayna Nyange ambaye anakua kwa kasi katika tasnia ya muziki ameibuka kuelezea kwanini analenga kupenya kwenye tasnia ya muziki ya Nigeria.

Dayna Nyange aliachia kollabo yake ya kwanza na Davido katika wimbo uliopewa jina la 'Ello' ambao ulipokelewa vizuri kati ya mashabiki wake.

Soma Pia: Dayna Nyange Afunguka Jinsi Alivyomshawishi Davido Kufanya Collabo Naye

Dayna katika mahojiano ya hivi karibuni ambayo alifanya alipofika Tanzania kutoka Nigeria, alifunua kwamba alikuwa ametumia muda mrefu kusoma muziki wa Nigeria. Aliongeza kuwa alikuwa amekaa karibu mwezi mzima nchini Nigeria kabla ya kusafiri kurudi Tanzania.

Dayna Nyange alielezea kuwa ni ngumu kwa mwanamuziki yeyote kufanikiwa Nigeria haswa kutoka Afrika Mashariki. Hata hivyo, alikuwa amejitolea kufanikiwa Afrika Magharibi kwa sababu tasnia yao ya muziki ndio iliyoendelea zaidi barani Afrika.

Soma Pia: Zuchu Nyimbo Mpya: Ngoma Tano Zilizomfanya Zuchu Kuwa Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki

Dayna alifichua kuwa wanamuziki wa Nigeria wana kipato kizuri kutokana na muziki wao, na kuongeza kuwa ni rahisi msanii kujiorodhesha kati ya watakaoongoza Afrika iwapo atashinda tasnia ya muziki ya Nigeria.

Dayna alikuwa mwanamuziki wa pili wa Kitanzania baada ya Diamond kutoa collabo na Davido.

"Tasnia ya muziki ya Nigeria imebanana sana. Sio rahisi kupenya. Yaani ukiona sisi watu ambao tunaowafahamu ukiwataja wasanii wa Nigeria, unaweza taja ata watano sita na wote wawe wanafanya vizuri.

"Lakini ukienda Nigeria ni tofauti sana, kwa hivyo mimi ni mtu ambaye nimekua nikienda kule na kurudi na nikasoma soko la kule," Dayna alisema.

Leave your comment