Tuzo za Muziki za MTV Afrika Kufanyika Tanzania Mwaka 2023

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Ngoma Zake Nandy Bila Malipo Kwenye Mdundo

Habari njema nchini Tanzania kwa sasa ni kuhusu waandaaji wa Tuzo za MTV Africa ambao wameamua kuichagua Tanzania kama nchi ambayo tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika kwa mwaka 2023.

Soma Pia: Diamond ‘Sona’, Alikiba ‘Mama’, Jux ‘Simuachi’ na Nyimbo Zingine Mpya Bongo Wiki Hii

Akitoa taarifa hizo ambazo zimepokelewa kwa mikono miwili na serikali ya Tanzania, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa na Utamaduni Bwana Saidi Yakub amesema kuwa serikali ya Tanzania tayari imeshafanya kikao cha kwanza kabisa na waandaaji wa tuzo hizo.

Bwana Yakub alisistiza kuwa Wizara ya Utamaduni na michezo iko tayari kushirikiana na MTV kuandaa tuzo hizo ambazo zilianza mwaka 2008.

Free Download: Pakua mixes 7 Kali za Clouds FM ndani ya Mdundo

"Kikao cha leo kimetupa fursa ya kuona namna gani Nchi yetu itafaidika na ujio wa Tuzo hizo, tumeona wasanii wetu watapata nafasi ya kujitangaza na kutangaza Sanaa ya Tanzania Duniani, Kuna fursa pia ya kutangaza Nchi yetu katika Utalii hivyo tumepokea wazo na tutalijadili na kutoa mrejesho wenye tija" alizungumza Bwana Yakub.

Kabelo Ngakane kutoka Afrika Kusini ambaye ni mwakilishi wa tuzo hizo amesema kuwa MTV wamevutiwa sana na Tanzania kwa sababu kwa sasa nchi hiyo imefunguka hivyo wameamua kufanya tuzo hizo Tanzania ili kuweza kuitangaza zaidi Tanzania huko duniani.

Mwaka 2021 waandaaji wa Tuzo hizo walipanga kufanya tuzo hizo huko Nchini Uganda lakini kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao waliamua kuahirisha tuzo hizo kwa mwaka 2021.

Mara ya mwisho kwa tuzo za MTV Africa kufanyika ilikuwa ni 2015 ambapo msanii Diamond Platnumz aliweza kupeperusha vyema bendera ya Tanzania baada ya kushinda tuzo ya Mtumbuizaji bora wa kiume mbele ya wasanii wakubwa Afrika.

Kando na Tanzania, nchi nyingine ambazo tuzo hizo zishawahi kufanyika ni pamoja na Nigeria mwaka 2008 na 2010, 2009 zilifanyika huko Nairobi Kenya kisha 2014, 2015 na 2016 zilifanyika huko Afrika Kusini.

Leave your comment