Free Download: Pakua mixes 7 Kali za Clouds FM ndani ya Mdundo

[Picha: Instagram]

Pakua Mixes Zote Kali za Clouds FM Ndani ya Mdundo

Huku kampuni ya mziki Mdundo.com ikizundua shughuli nzima ya Dj Battle hivi karibuni,tunaendelea kukuandalia mixes nzuri kwa ajili ya burudani yako binafsi.

Hicyo kamatika nakala hii tunakupa fursa ya kupakua mixes zako pendwa zinazopatikana kwenye tovuti yetu na pia zitachezwa ndani ya redio ya Clouds Fm. Usipitwe!

Cheza Singeli 

Huu ni mziki halisi wa Tanzania huku mix hii ikiwajumuisha wasanii Meja Kunta akimshirikisha Lavalava kwa wimbo wao "Wanga","Halloo" kisha Mzee wa Bwax na Dakota wakiwa na wimbo "Kijuso na hatimaye Mczo Morfani akimshirikisha Balaa Mc kwa wimbo "Kumbe Tamu". Pakua mix hii ya Cheza Singeli bila malipo!

Bongo Mpya

Hii ni mziki wa bongo aina ya RnB kutoka kwa wasanii kama vile Bruce Melodie, Remedy, Nandy. Ipakue hapa ili uweze kujitumbuiza wewe na mpenzi wako.

Afrobeat

Katika kukuza na kuendelea kuzikubali kazi za wasanii wa Afrika kiujumla, tumekuandalia mix hii kali ya mziki wa Afrobeat kutoka Afrika Magharibi wa wasanii kama vile Omah Lay, Joeboy na Runtown. Usikise kuipakua hapa!

Bongo Ya Marioo, Jux na wengineo

Hii ni mix inayoleta kazi za wasnii wa bongo wakiwemo Marioo, Jux, Latinoh miongoni mwasanii wengine.

Amapiano Mpya

Mziki wa Amapiano hauwezi kosa kwenye sherehe hivyo basi tumekuandalia mix moja kali ndani ya Clouds Fm kwa ajili ya kukuburudisha wewe na rafiki zako. Ipakue hapa!

Singeli Tamu

Mzee wa Bwax, Sholo Mwamba, Mfalme Ninja ni miongoni mwa wasanii waliohusishwa kwenye hii mixtape kali utakayopenda kuipakua hapa. Hivi tutaendelea kukuza mziki wa Singeli.

Qaswida Za Mwezi

Tukiwa ndain ya mwezi mtukufu wa Ramadan, tovuti ya Mdundo.com imekuandalia Qaswida mahususi kwa ajili yako. Hapa waeza kupakua mziki huu wa Qaswida bila malipo yoyote.

Leave your comment