Diamond ‘Sona’, Alikiba ‘Mama’, Jux ‘Simuachi’ na Nyimbo Zingine Mpya Bongo Wiki Hii

[Picha: Kayfmusic]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Ngoma Zake Nandy Bila Malipo Kwenye Mdundo

Ukiwa unafuatilia kwa ukaribu muziki wa Bongo Fleva, utafahamu kuwa, wiki hii wasanii tofauti tofauti kutoka Tanzania waliweza kupamba na kuchangamsha na kupamba tasnia ya muziki kwa kuachia ngoma kali ambazo zimeweza kuburudisha masikio ya mashabiki nchini Tanzania. Zifuatazo ni orodha ya nyimbo mpya ambazo zimeachiwa na wasanii wa Tanzania wiki hii:

Soma Pia: Diamond 'Wonder', Killy 'Vumilia' na nyimbo zingine Mpya Kutoka Tanzania

Niamini - Hamadai ft Alikiba

Hamadai na Alikiba wiki hii walichangamsha Bongo Fleva na ngoma yao ya ‘Niamini’ ambayo ndani yake wawili hawa wanaimba kwa hisia na bashasha huku wakiwataka wenzi wao kuwaamini katika mambo mbalimbali ambayo wanataka kuwafanyia ikiwemo kuwavisha pete na ahadi kedekede

https://www.youtube.com/watch?v=PunTEG27y58

Sona (Video) - Diamond Platnumz

Baada ya Wonder, wiki hii Diamond Platnumz aliamua kuachia video ya Sona ambayo imeongozwa na TG Omori ikiwa ni video ya nne kutoka kwenye EP First Of All ambayo iliingia sokoni takriban miezi miwili iliyopita.

https://www.youtube.com/watch?v=zpSj2Z2tbOg

Vimepanda Bei - B2K ft Mtafya

Ubunifu wa B2K umezidi kudhihirika, baada ya kuachia ngoma yake ya Vimepanda Bei ambayo ndani yake ameongea mambo ya msingi akigusia hasa mfumuko wa bei ambao unaendelea hapa nchini Tanzania kwa sasa, kitu ambacho kimegusa sana wasikilizaji wa ngoma hii.

https://www.youtube.com/watch?v=QN9A-3BrDUg

Simuachi - Jux

Juma Jux ameendelea kukoleza dozi ya burudani baada ya kuachia ngoma yake nzuri ya mapenzi ya kuitwa Simuachi ikiwa ni ngoma yake ya pili kwa mwaka huu wa 2022. Kama kawaida yake kuanzia mashahiri, mdundo mpaka midondoki ya ngoma hii, Jux ameweza kuitendea, haki.

https://www.youtube.com/watch?v=g4M0j30aWb8

Mama (Video) - Alikiba

Alikiba ameonesha uzalendo kwa nchi yake ya Tanzania, kupitia ngoma hii ya kuitwa "Mama" ambayo kwenye mashahiri ya wimbo huu, Alikiba anasheherekea mafanikio ya Rais Samia Suluhu Hassan tangu awe Rais wa Tanzania na kumpongeza Rais huyo kwa kuja na filamu ya Royal Tour.

https://www.youtube.com/watch?v=bEMPEgRrG_M

Cheusi Cheupe - Ommy Dimpoz ft Meja Kunta

Muziki wa singeli unaendelea kushika kasi nchini Tanzania na hii inaoneshwa na msanii Ommy Dimpoz ambaye ameachia ngoma yake kali ya singeli ya kuitwa Cheusi Cheupe ambapo ndani yake anajaribu kumshawishi mwanamke aweze kutoka nae kimapenzi. Ngoma hii amemshirikisha fundi wa singeli wa kuitwa Meja Kunta.

https://www.youtube.com/watch?v=bbTArJz7EvY

Star (Video) - Mabantu 

Baada ya subira ya muda mrefu hatimaye kundi la Mabantu limeachia video ya ngoma yao ya kuitwa ‘Star’ ambayo mitindo yadansi au kucheza pamoja ubora wa picha imeweza kupamba na kufanya kazi ya wasanii hawa kuwa ya kipekee sana.

https://www.youtube.com/watch?v=qouV6-c8Qrw

Leave your comment