Diamond 'Wonder', Killy 'Vumilia' na nyimbo zingine Mpya Kutoka Tanzania

[Picha:Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pakua Ngoma Zake Nandy Bila Malipo Kwenye Mdundo

Wasanii kutoka Tanzania wanaendelea kudhihirisha ubabe wao katika sanaa ya mziki kila wiki.

Ndani ya wiki hii wasanii kama vile Nay wa Mitego, Diamond Platnumz, Killy na wengineo wameachia kazi mpya na tunakupea fursa kuzitazama na kujipakulia polepole.

Pakua Mixes Maalum Kwa Ajili Ya Mwezi Mtukufu wa Ramadan

Wonder -Diamond Platnumz

Huku akiendeleaz ziara yake kule Uingereza Diamond Platnumz ameachia video mpya kutoka kwa ep yake 'First Of All' ya wimbo Wonder. Kwenye video diamond amepeleka posa kwa wazazi wa mpenzi wake waliokutana kupitia mtandao wa Instagram. Video hii ina uzuri wa picha huku maudhui yake ikionyesha mila na tamaduni za Nigeria. Hata kkwenye mistari yake Diamond anachukua mtindo wa Afrobeats na kweli kabisa shabiki zake wameipokea kazi hii kwa ukubwa sana. Tazama hapa:

https://www.youtube.com/watch?v=MiMPut0PjVw

Jiangalie -Dvoice FT Nay Wa Mitego

Huu ni wimbo singeli amabapo Dvoice amemshirikisha msanii wa Hip hop Nay Wa Mitego. Huu ni wimbo unaangazia mtu mwenye hulka za kupotosha na wanamuomba ajiangalie na abadilishe tabia zake.

Vumilia- Killy

Hii ni kazi yake Killy kutoka kwenye Ep Yake 'GreenLight' aliyoachia hivi karibuni. Vumilia ni wimbo unaongazia hisia zake kwa mpenzi wake huku akimuomba avumilie maisha anayompa. Kutoka Kondegang Killy anaendelea 

kuachia kazi mpya huku mashabiki wakipendezwa na ujuzi wake katika mziki.

https://www.youtube.com/watch?v=edtWG7DSQYU

Baby Hello -Nedy Musc FT Sultan King

Huu ni wimbo wa mapenzi ambapo Nedy namsifia mpenzi wake huku akimuomba amvumile na ajue kuwa nampenda yeye pekee.

Naogopa -Marioo Ft Harmonize

Naogopa ni kazi mpya kutoka kwa Marioo akimshirikisha bosi wa Konde Music Worldwide Harmonize. Huu ni wimbo unaoangazia hisia za Mapenzi. Wawili hao wanaonyesha ugwiji wao na ushairi mzuri humu huku video yake ikitarajiwa hivi karibuni.

https://www.youtube.com/watch?v=DytuZAZrE78

 

 

 

Leave your comment