Pakua Mixes Maalum Kwa Ajili Ya Mwezi Mtukufu wa Ramadan
8 April 2022
[Picha:Mdundo.com]
Pakua Qaswida Ya Mwezi ndani ya Mdundo
Kampuni ya muziki ya Mdundo Music imetangaza kuwawezesha Waumini wa dini ya kiislamu kwenye mwezi huu mtukufu wa Ramadhan kusikiliza orodha maalum ya muziki wa kaswida kuanzia Aprili 1 – 30 msimu huu wa Ramadhan, kila siku ambapo mdundo.com inatoa fursa ya kipekee kwa Waumini hao kupakua mpangilio wa muziki maalum wa Kaswida kutoka kwa maDJ mbalimbali kukuza safari yao ya kiroho.
Ramadhan 1
"Hii ni njia yetu ya kuwatakia ndugu zetu Waislamu Ramadhan Kareem – kwa kuwapa fursa ya kipekee ya kutiririsha, kusikiliza na kupakua muziki wa Kaswida na kupata maudhui mengine ya aina mbali mbali kwa gharama nafuu kupitia huduma yetu bora zaidi ya mziki mtandaoni - Mdundo.com," almesema Meneja Masoko wa kampuni hiyo Afrika Mashariki, William Abagi.
Qaswida Ya Ramadhan 2
Kupitia kushirikiana na wadau mbali mbali Mdundo imetuma ujumbe wa shughuli hii nzima kwa kupitia mitandao ya Millard Ayo, Bongo 5,na Mwananchi Scoop kujulisha jamii za Watanzania.
Akitangaza uzinduzi huo jijini Dar es Salaam, Meneja Miradi wa kampuni hiyo, Frida Muraguli amesema ofa hiyo ya kwanza na ya kipekee ipo wazi kwa waumini wa dini zote ikiwemo wapenzi wengine wote wa muziki.
Amesema fursa hiyo itawawezesha wateja kupata moja kwa moja muziki mchanganyiko kutoka kwa MaDJ maalum kwa bei nafuu ya sh.100, sh.500 au sh. 3,000 - kwa siku, wiki au mwezi kupitia Mdundo.com.
Qaswida Special
Katika fursa huyo, Clouds FM pia wameungana na Mdundo.com kuwapa wasikilizaji muziki mchanganyiko kutoka kwa MaDJ maarufu wa Clouds FM, ambao sasa unapatikana kupitia ukurasa wa Clouds FM.
Amesisitiza kuwa ukuaji wa kasi wa huduma za kutiririsha na kupakua muziki mtandaoni kumeifanya Mdundo.com kuwekeza muda, jitihada na teknologia nyingi zaidi ili kuwainua wasanii wa kitanzania.
"Mamilioni ya watumiaji wa mtandao kutoka ndani na nje ya nchi wanatumia huduma hiyo kusikiliza na kupakua muziki wa wasanii mbalimbali wa ndani na nje ya nchi.
Aidha, maudhui husika yanajumuisha aina mbali mbali za muziki ikiwemo Kaswida, Taarab, Singeli, Injili, Bongo, Naija/Afrobeat, Amapiano, Hip hop na nyingine nyingi.
Pakua Orodha mbali mbali ya mziki wa Qaswida hapa:
Qaswida Ya Mwezi
Qaswida Mpya
Leave your comment